Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipanda mti aina ya Mfenesi
katika moja ya nyumba zilizojengwa kupitia Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa
Umma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango huo iliyofanyika katika eneo la
Njedengwa Mkoani Dodoma tarehe 11 Desemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule pamoja na viongozi mbalimbali wakivuta kitambaa kwenye Uwekaji Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma katika eneo la Njedengwa Mkoani Dodoma tarehe 11 Desemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais - Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule pamoja na viongozi mbalimbali
wakitembelea mtaa wa Utumishi ambao umejengwa nyumba mbalimbali kwaajili ya
Watumishi wa Umma uliopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma wakati wa Uzinduzi wa
Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma tarehe 11 Desemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma katika wa hafla iliyofanyika eneo la Njedengwa Mkoani Dodoma tarehe 11 Desemba 2024.
No comments:
Post a Comment