Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi Kichama Mhe. Fatma Ramadhan Mandoba amewataka Wanachama wa Chama cha Mapindizi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Viongozi wao katika kuimarisha Chama na kuwaletea maendeleo Wananchi.
Ameyasema hayo huko Mwera Minanasini Wilaya ya Magharibi 'A' wakati akikabidhi Mifuko ya Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Maskan ya Mwera Minanasini.
Amesema Wanachama hao, iwapo watadumisha Upendo, Umoja na Mshikamano wataweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuongeza idadi ya Wanachama wanaojiunga na Chama hicho.
"Uchaguzi ni namba, hatuwezi kuendelea kushinda bila ya kuwa na idadi kubwa ya Wanachama, watakaoweza kukipigia kura Chama Chetu ifikapo 2025 ili kiendelee kushika Dola” alisema Mwakilishi huyo.
Amesema Chama cha Mapinduzi ni Chama imara na kipo msatari wa mbele katika kutekeleza ahadi zake kwa Wananchi na kuwaomba Wananchi kuendelea kukiamini na kukiunga mkono ili kiendelee kuwatumikia Wananchi.
Aidha aliwapongeza Viongozi na Wanachama wa Maskani ya Minanasini kwa kuamua kuanzisha Maskani hiyo jambo ambalo limewaunganisha pamoja na kuimarisha uhai wa Chama na Jumuiya zake.
Wakati huo huo Mhe. Mandoba alikabidhi Fedha taslim kwa Uongozi wa UWT Jimbo la Mtoni ili waewze kuongeza Mitaji ya vikundi vya Ujasiriamali walivyovianzisha.
No comments:
Post a Comment