Habari za Punde

Mafanikio ya Zanzibar Heroes kuna kila sababu kwa Serikali Kuendelea na UjenzI wa Academy za Soka Kila Mkoa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar, katika hafla ya kuwapongeza Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kwa kutowa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup 2025, kwa kuifunga Timu ya Taifa ya Burkina Faso katika mchezo wa Fainali uliyofanyika katika uwanja wa Gombani Chakechake Pemba 13-1-2025, wakati wa hafla ya chakula maalumu alichowaandalia katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-1-2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk,Hussein  Ali Mwinyi ameizawadia  Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes Shilingi Milioni 50 baada ya kulitwaa Kombe la Mapinduzi 2025 .

Akizungumza  katika Hafla Maalum ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya Wachezaji   wa Timu hiyo katika Viwanja Vya Ikulu, Rais Dk, Mwinyi  ameeeleza kuwa  timu hiyo imeiletea Heshima kubwa Zanzibar na Kudhihirisha Kuwa kuna Vipaji vingi vya Soka hapa nchini vinavopaswa Kuendelezwa katika Maeneo mbalimbali..

Dk,,Mwinyi  Amefahamisha kuwa  kwa Mafanikio ya  Zanzibar Heroes kuna  kila sababu  kwa Serikali  Kuendelea na UjenzI wa Academy za Soka Kila Mkoa  kwa Lengo la.Kuviibua Vipaji vya Vijana.

Rais Dk, Mwinyi ametangaza Dhamira  ya Kuunda Kamati Maalum ya Kitaifa hivi  karibuni itakayokuwa na Jukumu la  Kumshauri Namna Bora ya  kuuendeleza Mpira wa Miguu hapa nchini.

Dk,,Mwinyi ameeleza kuwa Hatua za Timu za Zanzibar Kulibakisha Kombe la Mapinduzi kwa  Mwaka wa Tatu Mfululizo  kunaashiria Uwezo Mkubwa wa Soka na Vipaji  viliopo .

"Wengi tulishtuka tuliposikia Timu za Afrika Magharibi zinakuja Kushiriki Michuano  ya Mapinduzi,Lakini Mumefanya kazi Nzuri Ahsanteni sana " alisema Dk,Mwinyi

Rais Dk, Mwinyi amefahamisha kuwa Tayari  Wagunduzi wa Vipaji vya Soka (SCOUT) wa Nchini Uturuki wameonesha nia ya kuja Zanzibar baada ya Kuushuhudia  Mchezo wa Fainali baina ya  Zanzibar na Burkinafaso na kukiri Kuwepo Vipaji Vingi.

DK, Mwinyi amesisitiza kuwa Lengo ni kuwa na Timu Imara za Mpira wa Miguu  katika ngazi zote zitakazoiletea heshima Zanzibar.

Rais wa Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) Suleiman Mahmoud Jabir alitumia Fursa hiyo Kumkabidhi  Rais Mwinyi Kombe la Mapinduzi 2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.