RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi,
akimkabidhi fedha tasilimu shilingi milioni 50 Nahodha wa Timu ya Taifa ya
Zanzibar Heroes Feisal Salum (Feitoto) wakati wa hafla ya kuipongeza Timu ya Taifa
ya Zanzibar Heroes kwa kutowa Kombe la Mapinduzi Cup 2025, katika mchezo wa
fainali na Timu ya Taifa ya Burkina Faso, uliyofanyika katika uwanja wa Gombani
Chakechake Pemba 13-1-2025 na kuibuka kwa ushindi wa bao 2-1, wakati wa hafla
ya chakula maalumu alichowaandalia katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar
leo.15-1-2025.
WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes
wakiwa na Kocha Mkuu wa Timu hiyo Hemed Moroco (kushoto) wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)
akihutubia wakati wa hafla ya Chakula Maalumu alichowaandaliwa katika viwanja
vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-1-2025, kwa ajili ya kuwapongeza kwa kutowa Kombe
la Mapinduzi kwa mwaka 2025, katika mchezo wa fainali na kuifunga Timu ya Taifa
ya Bukinafaso, mchezo uliofanyika Uwanja wa Gombani Chakechake Pemba 13-1-2025,
kwa ushindi wa bao 2-1.
No comments:
Post a Comment