Zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura awamu ya pili limekwenda vizuri katika Wilaya ya Kaskazi A’ ambapo wananchi walio wengi wamejitokeza kujiandikisha katika daftari hilo ili kupata haki yao ya msingi.
Akizungumza mzra baada ya kutembelea vituo vya uandikishaji wa daftari hilo Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe, Jaji Aziza Idd Suwed amesema kuwa zoezi lilifanyika kwa Amani na utuli na kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa katika daftari alipata haki yake ufanikiwa kuwaingiza katika mfumo.
“Tunashukuru zoezi limekwenda vizuri na hadi sasa hakuna matatizo yoyote ambayo yamejitokeza isipokua changamoto ndogondogo za wananchi wenyewe kutokana na vidole lakini tumeweza kuzitatua tunashkuru,”alisema Makamu kukesho Febuary 25.
Amesema Tume inaendelea na zoezi la uwandikishaji wa daftari hilo ambapo kesho wanatarajia kuanza Wilaya ya Kasazini B’ ili wananchi wa huko wapate haki yao ya msingi.
Aidha amefahamisha kuwa zoezi la kuvitembelea vituo hivyo limeanza Jumamosi na kuendelea hadi kufikia leo Febuary 24 ambapo wamefanikiwa kutembelea vituo13 kwa zoni ya Mkwajuni.
Hata hivyo Jaji Aziza amewashajiisha wananchi w Wilaya nyengine kujitokeza na kujiandaa kujiiandikisha katika daftari hilo.
Nao Wakuu wa Vituo vya kujiandikisha akiwemo Sabra Mhamed Khamis kutoka Kibeni na Miza Juma Haji kutoka Moga wamefahamisha kuwa tangu kuanza zoezi hilo hakuna tatizo lolote lililojitokeza kwai wamekwenda vizuri hadi kukamilika kwake.
Zoezi la uandikshaji wa daftari la wapiga kura linaendelea kesho katika Wilaya ya Kaskazini B’ambapo kwa leo limekamilika katika Wilaya ya Kaskazini A’katika vituo mbaimbali iikiwemo Kivunge,Kibeni,Chaanikubwa,
No comments:
Post a Comment