Habari za Punde

Serikali itaendelea kujenga Masoko zaidi ili kutoa fursa pana ya kufanya Biashara katika Mazingira mazuri.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi  amewahakikishia Wafanyabishara kuwa Serikali itaendelea kujenga Masoko zaidi ili kutoa fursa pana ya  kufanya Biashara katika Mazingira mazuri.

Rais Dkt, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipotembelea Masoko Ya Jumbi ,Mwanakwerekwe na Darajani  kuangalia Mwenendo wa Biashara  na Upatikanaji wa Bdhaa za Vyakula  kuelekea Mwezi Wa Ramadhani.

Dkt, Mwinyi  Ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa Ajili ya Ujenzi wa Masoko mengine Maeneo mbalimbali ili kila Mfanyabiashara afanye Biashara  kwenye Mazingira   rasmi .

Amewasisitiza Wafanyabishara kuepuka kufanya Biashara Barabarani na kufuata  utaratibu  uliowekwa na  Serikali hivi sasa.

Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuridhishwa  na Upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula na kuwataka Wafanyabiashara Kutopandisha Bei  wakati Ramadhani Itakapoanza.

Kuhusu Suala la  Usafi wa Masoko ameuagiza Uongozi wa Masoko hayo kutafuta njia Bora zaidi ya Uhifadhi wa Bidhaa za Wafanyabiashara ili Masoko kuwa safi wakati Wote.

Amezielekeza Taasisi zinazosimamia Masoko hayo kuhakikisha Upatikanaji wa  Huduma ya Maji  na Vipooza hewa katika Masoko yote pamoja  na kuimarisha Usafi.

Ziara hiyo ya Rais Dkt, Mwinyi ni ya Kwanza tangu kufunguliwa kwa Masoko Mapya ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Ukarabati Mkubwa wa Soko la Darajani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.