
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akiwa katika ukumbi wa New Amaan Complex Zanzibar wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Viongozi mbali mbali, Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali ya SMT na SMZ kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika hafla ya Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Ishirini(20) cha Maafisa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa New Amaani Hotel Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Viongozi mbali mbali, Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali ya SMT na SMZ kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika hafla ya Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Ishirini(20) cha Maafisa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa New Amaani Hotel Zanzibar.

Viongozi mbali mbali, Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali ya SMT na SMZ, wakimsikiliza Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akifungua mkutano huo kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika hafla ya Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Ishirini(20) cha Maafisa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa New Amaani Hotel Zanzibar.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR) Tarehe 03.04.2025
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema Maafisa Habari wa Serikali bado wana wajibu wa kuongeza juhudi katika kutangaza shughuli na miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali yenye leng la kustawisha maisha ya Mtanzania na kutokomeza umasikini.
Ameyasema hayo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Ishirini(20) cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikalini iliyofanyika katika Ukumbi wa New Amaani Hotel, Zanzibar.
Amesema Serikali zinaendelea kutekeleza na kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo Sekta ya Afya, michezo, elimu, uvuvi, kilimo, nishati, miundombinu ya barabara,viwanda na mengineyo ambayo inahitaji mchango mkubwa wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika kufikisha taarifa kwa jamii juu ya kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Maafisa Habari na uhusiano wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanatoa taarifa zenye kuimarisha demokrasia, utawala bora, haki za binaadamu, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi pamoja na kuripoti taarifa za udhalilishaji wa ina zote.
Aidha, Mhe.Hemed amefahamisha kuwa Maafisa Habari na Mawasiliano wanapaswa kuandaa taarifa zitakazoimarisha huduma na kulinda haki kwa makundi maalum wakiwemo wanawake, vijana,wazee, watoto na watu wenye ulemavu ili kuweza kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameziagiza Taasisi zote za Serikali za SMT na SMZ kuhakikisha zinaandaa Mikakati Imara ya Mawasiliano pamoja na kuajiri maafisa habari na mawasiliano watakaotumika kama washauri wa masuali ya mawasiliano kwa Umma pamoja na kuwa daraja la mawasiliano kati ya Serikali na wananchi.
Amezitaka Wizara na Taasisi za Serikali kutenga bajeti ya kutosha ya kununulia vitendea kazi na kugharamia shughuli za mawasiliano ya Serikali kwa Umma pamoja na kuwajengea uwezo kitaaluma ili waweze kutumia Teknolojia ya kisasa katika utekelezaji wa majukumu yao ya mawasiliano kwa Umma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na watendaji wote wa Taasisi zote za Serikali kushiriki kikamilifu katika kutangaza shughuli za Serikali, kujenga uhusiano mzuri na waandishi wa habari pamoja na kuwashirikisha kwenye shughili zote za miradi ya maendeleo ili waweze kutoa ushauri wa kitaaluma na namna bora ya kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Nae Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Palamagamba Aidan Kabudi amesema lengo la kufanyika kwa kikao kazi cha 20 cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali ni kutoa fursa ya kubadilishana mawazo na kujifunza mambo mbali mbali yahusuyu Tasnia ya habari hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020-2025.
Kabudi amesema katika kikao kazi hicho washiriki watajengewa uwezo kitaaluma juu ya namna bora ya kutangaza habari za Serikali hasa taarifa za miradi inayotekelezwa na Serikali zote mbili yenye lengo la kuwaondolea changamoto wananchi wake.
Profesa Kabudi amesema mbali na kikao hicho, Maafisa Habari watapata fursa ya kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii vilivyopo zanzibar na kuvitangaza pamoja na kupanda miti zaidi ya elfu mbili (2000) katika Msitu wa Muyuni na Msitu wa Jambiani iliyoko Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kulinda na kutunza mazingira mazuri.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya SMT Ndugu Gerson Msigwa amesema madhumuni ya Kufanyika kwa Vikao kazi kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali ni kutekeleza malengo mahsusi ya kuimarisha mawasiliano kwa Umma na kujenga uhusiano mzuri kati ya Maafisa Habari na Viongozi mbali mbali wa Serikali na jamii kwa ujumla.
Msigwa amesema kukutana pamoja kwa Maafisa Habari wa Serikali wa pande zote mbili za Muungano kunatanuwa wigo mpana wa mafundo na mazingatio kwa Maafisa Habari sambamba na kuchochea kuimarika kwa Muungano wa Tanzania.
Msigwa amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali kuyatumia vyema mafunzo waliyopatiwa ambayo yatawasaidia katika kuboresha utendaji kazi wao na kufanya kazi zao kwa ufanisi na uweledi mkubwa.
Kwa upande wao Washiriki wa Kikao kazi hicho wamesema mafunzo wanayoyapata yanawajengea uwezo wa kujiamini katika kufanya kazi zao kwa uweli pamoja na kujenga ushirikiano wa kikazi kati ya pande mbili za Muungano.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Tarehe 03.04.2025.
No comments:
Post a Comment