MBUNGE wa Jimbo la Njombe mjini mkoani humo,Mhe.Deodatus Mwanyika amesema shida kubwa iliyokuwa inawakabili wananchi wa Njombe mjini ukosefu wa maji safi na salama,hii inatokana na ufinyu wa bajeti uliokuwepo katika Sekta ya Maji.
Mwanyika amesema lakini ndani ya kipindi cha Miaka minne ya uongozi wake Rais Dkt Samia Suluhu Hassan miradi mikubwa Minne ya Maji imetekelezwa ambapo miwili imeshakamilika na inatoa Maji katika Mji wa Njombe nakupelekea changamoto hiyo kumalizika.
Akichangia Bungeni jijini Dodoma hotuba ya Bajeti kuu ya Serikali ya Ofisi ya Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mwanyika alisema,wannachi wa Jimbo la Njombe Mjini ni mashuhuda wa mafanikio makubwa yaSerikali ya awamu ya sita ambayo imepeleka fedha nyingi kwa ajili ya kuwasogezea huduma mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu katika sekta ya Elimu,Maji,Afya, Usafiri wa Reli pamoja na Usafiri wa Anga.
Alisema miaka ya nyuma kulikuwa na uhaba wa maji lakini hivi sasa baada ya Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ikiwemo kuboresha miundombinu katika sekta ya maji,wananchi wameanza kuonja matunda ya uwekezaji mkubwa wa miradi hivyo iliyotekelwzwa na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali Jimboni humo yenye zaidi ya Bilioni 67.
Aidha Mwanyika alieleza kuwa changamoto mkubwa inayoikanili Njombe Mjini ni kutengeneza ajira, Njombe inategemea Kilimo kwa Asilimia 99 ambacho ni Mazao ya Chakula, Mazao ya Biashara na Mazao ya Misitu na kuitaka Serikali kuhakikisha zao la chair ambalo ndio uwekezaji mkubwa mkoani Njombe linapewa kipaumbele ili kuwawezesha vijana wengi kujiajiri kupitia kilimo.
"Waziri Mkuu amekuja Njombe zaidi ya mara mbili na mara zote amekuwa akishughulika na changamoto ya uwekezaji.Sekta ya Uwekezaji kwenye Kilimo cha Chai ndiyo uwekezaji mkubwa Njombe lakini kuanzia Mwaka 2018 Sekta hii imedolola (Imekwama) kutokana na na kukosekana kwa umakini katika kutafuta Wawekezaji kumekuwa na changamoto ya kukosekana kwa ajira maeneo ya Vijijini;
"Tunahitaji ajira, tunahitaji kodi na tunahitaji mazao ya kupeleka nje ya nchi tupate fedha za kigeni. Wawekezaji wa Chai wa kampuni ya DIEL umekuwa ni mwiba mkubwa sana kwa wananchi wa Njombe. Serikali iwe tayari kufanya maamuzi magumu kwa wawekezaji wa aina hii ambao wanapewa ardhi (Productive Assets) kama haitumiki kuzalisha ajira na kuzalisha bidhaa na kuleta fedha za kigeni maana yake hatuitumii kustawisha maisha ya wananchi wetu"Alisema Mwanyika.
Katika hatua nyingine,Mwanyika alieleza kuwa sekta ya Misitu ni sekta muhimu inayotoa ajira kwa wingi na mkoa wa Njombe una kampuni kubwa ya Kibena ambayo ni mfano halisi wa Kampuni ya uwekezaji maeneo ya Njombe na maeneo mengine ya Tanzania. Ni kampuni ambayo inazalisha ajira kutokana na kuotesha Mazao (Plantations) , ikipewa ardhi itaweza kutoa ajira nyingi kwa Vijana wengi wa Kitanzania wakiwemo wazawa wa mkoa wa Njombe.
"Serikali ina jukumu la kuwalinda wananchi wake kuhakikisha wawekezaji hawapewi vibali vya kukata miti hovyo. Kuna mpango mkakati wa mwaka 2021 - 2030 wa kuongeza thamani kwenye Mazao ya Misitu, kuna GN ya 2023 namba 2.2.1 inayoruhusu Usafirishaji wa Malighafi za Misitu kwenda nje ya nchi. Tunaitaka Serikali kutumia GN kuzuia kutoa vibali kwa wawekezaji wa aina hii" Alisisitiza Mwanyika.
No comments:
Post a Comment