Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mmiliki wa Klabu ya
Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11
Aprili, 2025. Katika
mazungumzo yao Rais Dkt. Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi
yake ya Six Rivers ambayo ina shughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya
vizuri katika kudhibiti muingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana
na Shirika la
Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti
wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
Kupitia Taasisi yake ya Six Rivers, Sir Jim Ratcliffe amebainisha kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kurejesha hadhi ya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya mpira wa Miguu
ya Manchester United ya Uingereza iliyosainiwa na Wachezaji wa Timu hiyo kutoka
kwa Mmiliki wa Klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11
Aprili, 2025. Mmiliki
wa Klabu hiyo Sir Jim
Ratcliffe ameeleza dhamira yake ya kuitumia Klabu yake kutangaza utalii nchini
Tanzania. Rais
Dkt. Samia pia amemkaribisha Mmiliki huyo wa Club ya Manchester kuanzisha Vituo
vya Mafunzo ya Michezo (Sports Academy) hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya mpira wa miguu
kutoka kwa Sir Jim Ratcliffe Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United
ya Uingereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment