Na Mwantanga Juma Maelezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Dkt. Harouna Ali Suleiman ameviomba vyombo vya Sheria kuhakikisha wanatenda haki ili suluhu zipatikane hasa Kwa migogoro ya ardhi.
Akizindua kampeni ya Msaada wa kisheria ya mama Samia mkoa wa kaskazini unguja katika uwanja wa Tumaini Mkwajuni amesema kutokana na kilio Cha muda mrefu Kwa wananchi kunyimwa haki zao hivyo Kwa kampeni hii timu za wataalamu zitaweza kuwasikiliza katika masuala mbalimbali yakiwemo ya jinsia na migogoro ya ardhi.
Amesema Matarajio baada ya kukamilika Kwa utekelezaji wa kampeni hiyo ni kupata uelewa zaidi Kwa wananchi kuhusu upatikanaji wa haki, mifumo ya kisheria iliopo, haki za binaadam na makundi maalumu.
Dkt. Mw. Harouna amefahamisha kwamba kampeni hiyo inatarajiwa kufikia asilimia 75 katika utoaji wa huduma za wananchi hadi Sasa kampeni imewafikia wananchi takriban 1246 Kwa mikoa iliozinduliwa.
"masheha kutokujiingiza katika migogoro ya kisheria ambayo hawana elimu nayo na badala yake kuwapeleka wananchi kwenye vyombo husika Kwa kupata ufafanuzi zaidi" alisisitiza Dkt. Harouna.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya katiba na sheria Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Franklin Rwezimula amesema kampeni hiyo imekuwa na muitikio mkubwa Kwa walengwa na kusaidia kutatua matatizo mbalimbali ya kisheria Kwa wananchi Kwa kupelekwa mashauri yao mahakamani Kwa wakati na kwa haraka zaidi.
Aidha Rwezimula amesema Wizara imepewa dhamana ya jukumu la kutoa msaada wa kisheria nchini Kwa wananchi kupata haki zao za kisheria.
Akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja mhe. Mattar Zahor Masoud amesema kampeni hiyo Kwa kaskazini ni msaada mkubwa Kwa wananchi kupata msaada huo bure Kwa siku 9.
Amesema mkoa wa kaskazini umegubikwa na changamoto nyingi hasa migogoro ya ardhi hivyo kampeni hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kupunguza malalamiko ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya
Amewataka uongozi wa Mkoa utahakikisha unasimamia katika kuwahamasisha wananchi kuyafikia maeneo hayo yanayotolewa huduma Kwa takriban siku zote 9 ndani ya Mkoa huo.
kampeni hiyo ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya mama Samia Leo imezinduliwa Katika Mkoa wa Kaskazini Unguja huku ikibakisha Mikoa miwili Kwa Zanzibar ambayo ni kusini Unguja na Kusini Pemba imebeba kauli mbiu isemayo msaada wa kisheria Kwa haki, usawa, amani na maendeleo
No comments:
Post a Comment