Habari za Punde

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AIPONGEZA TANGA UWASA KWA MATUMIZI YA MITA ZA MALIPO KABLA KWA WANANCH


Na Oscar Assenga,TANGA
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) imepongezwa kwa kiongozi wa mbio wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt Samia Suluhu la ufungaji wa mita za maji za malipo kabla kwa wananchi lengo likiwa kuboresha utoaji wa huduma
Pongezi hizo zimetolewa leo na Kiongozi wa Mbio mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa Ufungaji wa Dira za Malipo kabla katika eneo la Mwakidila kata ya Tangasisi Jijini Tanga baada ya kupokea taarifa ya mradi na kujionea hali ya halisi ya utekelezaji wake.

Alisema kwamba amewapongeza kutokana na kwamba mamlaka hiyo kuwa wasikivu na kutekeleza agizo la MRais kwa mradi huo wa kimkakati unaoenda kuondosha changamoto ya muda mrefu ambayo walikuwa wakiipata wananchi ya malalamiko ya bili za maji.
Alisema kwamba mfumo huo sasa unaenda kuondosha lawama kwa viongozi kwani wananchi wanaenda kupata maji kulingana na uwezo wao hivyo kutokana na hilo wamehaidi kwenda kuwa mabalozi waziri kwa kuwasemea juu ya usimamizi wao mzuri wa mfumo huo kwa sababu unaenda kuwasaidia wananchi hivyo tunawashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi hii nzuri.
Awali akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi huu kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025,Meneja wa Ankara na Makusanyo wa Tanga Uwasa Francis Barabara alisema kwamba mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi Julai mwaka jana na una thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 1.87 na unatekelezwa kwa fedha za Serikali Kuu kupitia programu ya IFF-OBA na Mfuko wa Maji wa Taifa.
Francis alisema kwamba utekelezaji wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 55.05 kwa ufungaji wa dira 2,202 kati ya dira 4,000.
Aidha alisema utekelezaji wa mradi huu utaongeza Ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kupunguza madeni ya wateja, udhibiti wa upotevu wa maji, uimarishaji wa matumizi sahihi ya maji kwa wateja na hivyo kupunguza malalamiko ya bili za maji.

Akizungumza wakati mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua na kutembelea mradi huo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema maboresho kupitia mradi wa hati fungani ambao upo kwenye hatua ya utekelezaji una thamani ya Sh.Bilioni 53.

Alisema kwamba katika mradi huo wamedhamiria kuboresha miundombiniu kwenye chanzo cha maji bwawa la mabayani ambalo lilijengwa muda mrefu 1978 hivyo kutokufanyiwa ukarabati hivyo wameona walifanyie ukarabati ili liweze kuendana na uhitaji wa maji kwenye mji wa Tanga,Pangani na Mkinga.

Aliongeza kwamba hivyo wanarekebisha mtambo kwenye bwawa na katika pampu ambazo zinapeleka maji kwenye mtambo wa kutibu maji sehemu hiyo ikiwemo kurekebisha kuweka mabomba mapya na kutoka eneo hilo kupelekea mjini kuna bomba kubwa linalazwa .

Mwenyekiti huyo alisema kwamba hatua nyengine ni kusambaza maji kwenye mji wa Tanga na mabomba yaliyopo ni ya zamani yamechakaa na kama watafanikiwa presha itakuwa kubwa na mabomba ya zamani yanashindwa kuhimili na watarekebisha ili kuweza kuhimili na mradi huo mpaka Octaba mwaka huu utakuwa wamemaliza marekebishi na utaanza kufanya kazi.
Akizungumza mita za Luku, Dkt Fungo alisema kwamba matarajio yao ni kuhakikisha wananchi wanaunganishwa na nazo kwa wale ambao hawajafikiwa ambapo alisema kabla ya kufunga mita za luku kulikuwa na malalamiki sana kwa wateja kuona kama wanabambikiziwa bili kitu ambacho hakiwezekana.

Alisema lakini kwa kuondoa shida hiyo kwa wananchi na Rais alitoa maelekezo kuona njia bora ya kuweza kurekebisha dosari zilizojitokeza na hivyo njia bora wakaona ni mita za luku na walifanya majaribio kwa miaka miwili na sasa wamefikia mita ambazo zinaweza kukudhi mahitaji.

“Tumeanzaa na kuzifungwa kwa wateja wetu na na tulianza na mita 4000 na mpaka sasa tumefikia asilimia 60 wamefunga mita 2200 na tunatarajia kuzimaliza kwa kuwafungia watu wenye uhitaji na wale waliokuwa na madeni na muda mfupi tutakuwa tumezimaliza kwa wenye madeni”Alisema

Awali ya pili mradi wa Mradi wa Hat fungani utakuwa na mita 10,000 kwa hiyo wanataraji kuwafikia wananchi kwa wananchi wengi Tanga kutokana na mahitaji ni mengi kutokana wenye uhitaji wa kubadilishiwa mita za luku wana wateja kkaribia 50,000 bado wanaendeleaa kuomba na wanatarajiwa kufikia mpaka 75,000 na ubadilishaji wa mita utakuwa ni urtarbu wa kudumu wataweka za luku.

Kwa hiyo mita za zamani zitapeleekwa kwenye maeneo ambao hawajayafikia lengo kuhakikisha maeneo yote zinawekwa mita za kisasa,lengo kufiia asilimia 95 na maeneo mengine ni 85 na lengo ni kufikia asilia 100

MWISHO.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.