Na.Mwandishi Wetu.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini.
Waziri Mazrui ameyaeleza hayo huko Ofisini kwake wakati alipoagana na Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO aliyepo Zanzibar Dkt Ghirmay Andemichael mara baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.
Amesema katika kipindi chote cha miaka 10 alichofanya kazi hapa nchini alikuwa kiungo mzuri wa kutekeleza kazi mbali mbali za kuimarisha sekta ya afya ikiwemo suala zima la kupambana na maradhi ya uviko 19, maradhi ya miripuko, Chanjo, upatikanaji wa gesi pamoja na masuala mbali mbali ya kupambana na vifo vitokanavyo na uzazi, maradhi yasiombukiza na Malaria.
Aidha alifahamisha katika kupambana na maradhi yasiombukiza NCD Waziri Mazrui ameimba WHO kuchukua hatua za makusudi za kusaidia Zanzibar kukabiliana na maradhi hayo ili yasiendelee kuleta athari hapa nchini.
Sambamba na hilo ameomba kusaidia zaidi katika kuangalia ubora wa hewa tiba inayozalishwa katika Hospitali za hapa nchini kutimiza viwango vya WHO pamoja na suala la ukuwaji wa watoto na kufuatilia katika masuala ya ufuatiliaji wa maradhi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa WHO kwa Zanzibar ambae anaemaliza muda muda wake Dkt Ghirmay Andemichael amesema ataendelea kushirikina na Wizara ya Afya katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa Zanzibar.
Ameishauri Wizara ya Afya kwa kuangalia zaidi kuimarisha huduma katika vituo vya Afya kwa kuweka wafanyakazi wa kutosha, Vifaa tiba pamoja na dawa ili kukabilina na maradhi sambamba na huduma za Afya ya mama na mtoto.
Mwisho
No comments:
Post a Comment