Na.Mwandishi Wetu.
WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea ujumbe wa wataalamu kutoka nchi mbali mbali duniani ukiwa na lengo la kutoa mafunzo kwa watendaji wa Taasisi ya utafiti wa Afya ZAHRI wa kuimarisha huduma za afya.
Akizungumza mara baada ya kupokea ujumbe huo huko ofisini kwake Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui amesema wataalamu hao wamekuja na mbinu ya kutumia hesabu ya kuweza kutambua magonjwa mbali mbali yakiwemo maradhi yasiombukiza na maradhi ya kuambukiza.
Amefahamisha kuwa mafunzo hayo kwa wataalamu wazawa yatasaidia kufanikisha utoaji wa huduma za afya zenye ubora katika Taasisi ya utafiti wa afya katika kubaini magonjwa kwa haraka yanayowasumbua wananchi na kupatiwa ufumbuzi.
Aidha amesema katika kufanikisha mafunzo hayo Wizara ya Afya kupitia Taasisi ya Utafiti wa Afya wa ZAHRI kwa kushirikina na vyuo vikuu ikiwmo NANJING MEDICAL UNIVERSITY ya nchini China watafanikisha kutumia takwimu na taarifa ya kujikinga na maradhi mbali mbali kama vile Kichocho, Malaria na maradhi mengine.
Waziri Mazrui amesema ujio wa wataalamu hao utasaidia katika kupanga mikakati madhubuti ya kukabiliana na maradhi na kufanikisha utoaji wa huduma zenye ubora kwa wananchi mbali mbali wanaofika kupata huduma za afya Hospitali na vituo vya afya.
Ujumbe wataalamu uliofika hapa nchini ni pamoja na nchi ya China, Ethiopia, Cameroon, Kenya, Uganda Thailand .
No comments:
Post a Comment