Na Khadija Khamis, WHVUM. 21/07/2025.
Afisa Afya ya Jamii na Lishe kutoka ,Kitengo cha Maradhi Yasioambukiza Mnazi Mmoja Subira Bakari Ame amewataka Wagonjwa wanaoishi na Maradhi Yasioambukiza kutumia dawa kwa mujibu ya maelekezo ya Daktari ili kujiepusha kuingia katika athari zinazotokana na Maradhi hayo.
Ameyasema hayo katika Mkutano wa Ushawishi na Utetezi na kubadilishana uzoefu juu ya kupambana na maradhi yasioambukiza katika Muungano wa Jumuiya ya Maradhi yasioambukiza Zanzibar (Z-NCDA), Mpendae .
Amesema ni vyema Wagonjwa wa Maradhi hayo wajikubalishe kutumia dawa kwa usahihi ili kujiondoa katika athari zinazoweza Kujitokeza .
Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya pamoja na Wadau wa Maendeleo amejidhatiti kuratibu huduma za Maradhi hayo katika Vituo vya Afya 70 kwa Unguja na Pemba na Vikundi 52 vya wagonjwa wa Sukari na Presha ili kuwaondoshea usumbufu wananchi wake .
Nae Katibu wa Jumuiya ya watu Wanaoishi na Saratani Zuhura Abdalla Abdulkarim ameitaka Jamii Kujitokeza kwa wingi kupima Afya zao wanaposikia matangazo ya uchunguzi wa Afya kwani Saratani ikigundulika mapema inatibiwa na kupona .
"Wito wangu kwa wanawake wenzangu na wanaume pia wasidharau wakisikia Kuna uchunguzi wa Afya kwani Maradhi Yasioambukiza yameongezeka hususan Saratani ya Matiti, ,Shingo ya Kizazi pamoja na Tenzi Dume.tuwe tunafanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kujua Afya zetu."amesema Katibu Zuhura.
Serikali inachukuwa juhudi mbali mbali Kwa kuandaa Makongamano Mikutano pamoja na Mabonanza ya mara kwa mara yanayoambatana na Huduma ya uchunguzi wa Afya kwa wananchi hivyo ipo haja kuitumia fursa hiyo kujua Afya zao.
Kwa Upande wa Naibu Katibu wa Jumuiya ya Sickle Cell Zanzibar Halima Mohamed Salum ameishukuru Serikali kwa kuwapatia Jengo lao la Klinik ya Sickle Cell Ijitimai na kuomba kuwawekea na Pharmacy katika jengo hilo ili kuwaondoshea usumbufu .
Katibu Halima ameiyomba jamii kuchangia damu kwa wingi ili kuwasaidia Wagonjwa wa Sickle Cell, Akinamama Wajawazito pamoja na wanaopata ajali ili kuokoa Maisha yao .
Utafiti uliofanyika Mwaka 2011, Wagonjwa wa Sukari ilikuwa asilimia 3.7, kwa Mwaka 2023 umeongezeka kuwa asilimia 7.5, Kwa Upande wa shindikizo la damu (Presha) ilikuwa asilimia 33, 2011 na kufikia asilimia 43, 2023.
No comments:
Post a Comment