Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla Amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu Katika Sala ya Ijumaa Masjid Munawwar - Pemba

Makamu wa  Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na waumini wa Masjid Munauwara uliopo Mfikiwa Wilaya ya Chake- Chake Pemba mara baada ya kumalizika Kwa Ibada ya swala ya Ijumaa. Imetolewa na Kitengo cha Habari(OMPR) Tarehe 15.08.2025.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Alhajj Hemed Suleiman Abdulla, amewataka waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kwa ujumla kuondoa hofu katika kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Alhajj Hemed ameyasema hayo  wakati alipokuwa akisalimiana na waumini wa dini ya kiislamu katika Masjid Munauwara uliopo Mfikiwa Wilaya ya Chake-Chake Pemba mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya swala ya Ijumaa.

Amewataka waumini hao kuondosha chuki na uadui baina yao na kutokukubali kutumika vibaya kwa maslahi ya mtu binafsi  ama kikundi cha watu wasiopenda kuona Amani ndani  nchi inatawala.

Alhajj Hemed amefahamisha kuwa kuwepo kwa amani ma utulivu ni jambo la muhimu ili Seeikali na wananchi waweze kufanya mambo  ya malendeleo

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaasa wanasiasa kutumia vizuri majukwaa ya kisiasa kwa kuwataka wafuasi wao kuendelea kudumisha  amani iliyopo nchini.

Amewataka wazazi kuwasimani na kuwalea vijana wao katika maadili mema ili kuepuka kujihusha na matendo mabaya yanayomchukiza Allah lakinj pia yanayoweza  vunja Sheria za nchii.

Mhe. Hemed amewataka wananchii kuendelea kuwa wastahmilivu na  kutoa ushirikoano wakati wa ujenzi wa mieadi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Sambamba na hayo, ameeleza kuwa serikali itatowa fursa mbali mbali kwa vijana wanaoishi  karibu na uwanja huo na maeneo ya jirani ili kuweza kujiendeleza katika kimaisha.

Akitoa hotuba katika swala ya Ijuma, ustadh Khalifan Salim Omar amesema ili kuweza kupata msamaha mbele ya Allah ni lazima kujiepusha na kufanya matendo machafu yenye kumchukiza Mwenyezi Mungu.

Ustadhi Khalfan amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kuhimizana kufanya mambo mema na kukatazana mabaya jambo litakalozidisha umoja, upendo na mshikamano baina yetu.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Tarehe 15.08.2025

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.