Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika uzinduzi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na Barabara ya Mkoani- Chake Chake uliofanyika katika Viwanja vya uwanja wa Ndege Pemba.
Amesema ujenzi wa miradi hio ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025 ambapo malengo ya serikali ni kuhakikisha kuwa Pemba inakuwa na Uwanja wa ndege wa Kimataifa ambao utaifungua Pemba Kimataifa kwa kukuza utalii, uwekezaji na biashara.
Mhe. Hemed amefahamisha kuwa serikali imejipanga katika kuhakikisha barabara zote za Zanzibar zinajengwa kwa kiwango cha lami na kuwa katika hali nzuri kwa kuhakikisha zinafanyiwa marengenezo pale inapohitajika.
Aidha, Makamu wa Pili wa Rais amesema miradi hio itakapokamilika itapelekea kuimarika kwa huduma za usafiri wa anga na kuifungua Pemba kiuchumi kwa kuongezeka shughuli za kibiashara, kuimarika kwa sekta ya utalii itskayochangia kuongezeka kwa pato la Taifa na kupunguza umasikini wa kipato kwa wananchi.
Sambamba na hayo ametoa wito kwa Mkandarasi wa ujenzi wa uwanja huo kampuni ya PROPAV INFRASTRUCTURES na mshauri elekezi Dar Alhandasah Consultant kuifanya kazi hio kwa umakini na kea viwango vya Kimataifa n kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Mhe. Hemed amesema maendeleo yoyote yanahitaji kuwepo kwa Amani, Umoja na mshikamano hivyo amewaasa wazanzibari kuendelea kuidumisha amani iliyopo nchini pamoja na kuwataka kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili kuweza kufanikisha utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa maslahi ya nchi.
Kwa upande wake waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe.Dkt Khalid Salum Muhammed amesema Rais Dkt. Hussein Mwinyi amefhamiria kuifungua Pemba kiuchumi kwa kujengwa miradi mbali mbali ya maendeleo ikkiwemo ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na Barabara ya Mkoani Chake Chake.
Amesema Wizara ya Ujenzi inaendelea na ukarabati wa Bandari ya Mkoani ambayo itakuwa na uwezo wa kupikea meli kubwa kutoka nje ya nchi jambo litakalochochea ukuwaji wa uchumi kisiwani Pemba.
Akisoma taarifa ya kitaalamu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiano na Uchukuzi Dkt. Habiba Hassan Omar amesema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikichukua juhudi kubwa katika kuimarisha huduma za Usafiri wa Anga na Barabara kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuwandolea usumbufu wananchi na wageni wanaofika Zanzibar.
Dkt. Habiba amesema Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba umeanza rasmi Novemba 2024 na unatarajiwa kuchukua muda wa miezi 36 kumalizika kwake ambapo
Mkandarasi wa ujenzi wa Uwanja huo ni Kampuni ya PROPAV INFRASTRUCTURES kutoka nchini Hispania na Msimamizi wa ujenzi ni Kampuni ya DAR AL HANDASAH CONSULTANTS kutoka Lebanon unatarajiwa kugharimu jumla ya EURO Milioni 170.
Ujenzi wa Uwanja huo utahusisha Jengo jipya la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria wasiopungua laki tatu nanthelathini kwa mwaka ikiwemo abiria wa ndani (Domestic) na abiria wa kimataifa (International) pamoja na ujenzi wa Njia ya kuruka na kutua Ndege (Runway) yenye urefu wa mita 2,510 na upana wa mita 45 utakaokuwa na uwezo wa kutua ndege zote za aina ya Code 4C.
Kwa upande wa Utekelezaji wa Mradi wa barabara ya Mkoani – Chake-chake yenye urefu wa (43.5km) inayojengwa na Kampuni ya PROPAV INFRASTRUCTURES ya Hispania ikisimamiwa na Kampuni ya DAR AL HANDASAH CONSULTANTS ambayo inatarajiwa kuchukua muda wa miezi 36 hadi kumalizika kwake.
Ujenzi wa barabara ya Mkoani- Chake- Chake utagharimu zaidi ya EURO milioni 93 itakayohusisha njia za watembea kwa miguu, taa za barabarani (streetlights) pamoja na alama zote muhimu za usalama wa barabarani ambapo itakapokamilika itawarahisishia wananchi kuzifikia huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa urahisi pamoja na kuunganisha mji wa Mkoani ambapo kuna Bandari ya Mizigo na abiria ya Mkoani na Mji wa Chakechake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya PROPAV INFRASTRUCTURES Bwana Cristiano Becker amesema wanatambua kuwa uwanja wa ndege ni mlango mkuu na daraja la kuiuganisha Pemba na dunia hivyo ameahidi kuwa wataujenga uwanja huo kwa viwango na ubora unaokubalika Kimataifa.
Bwana Christiano amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeiamini Kampuni ya Propav Infrastructructures na kuipa mkataba wa kuujenga uwanja huo huvyo kampuni yake Itajenga Uwanja wa Ndege wenye hadhi na sifa zote za Kimataifa utakaoifungua Pemba kiuchumi na kiutalii.
Akizungumzia ujenzi wa barabara ya Mkoani- Chake Chake Bwana Christiano amesema ahadi yake ni kujenga barabara hio kwa uamifu mkubwa na yenye viwango vinavyoendana na mustakbali wa Pemba inayotakiwa itakayowavutia zaidi wawekezaji, kukuza uchumi na kuongezeka kwa ajira.
Amesema ujenzi wa Mradi wa Uwanja wa ndege wa Pemba pamoja na barabara ya Mkani- Chake Chake utatoa ajira zaidi ya elfu moja kwa wakaazi wa Pemba, wananchi kuoata fursa ya kufanya biashara ndogo ndogo pamoja na mafunzo nanujuzi kwa vijana watakaopata fursa ya kufanya kazi na kampuni ya PROPAV INFRASTRUCTURES.
Imetolewa na kitengo cha habari ( OMPR )
Leo tarehe 25 / 09 / 2025
No comments:
Post a Comment