Habari za Punde

Mtandao wa Polisi Wanaweke Songwe (TPF NET) Wawakumbuka kwa Dua Askari wa Kike Waliotangulia Mbele ya Haki

WhatsApp Image 2025-09-06 at 19.00.51_591fac23.jpg

Mwenyekiti wa Mtandao huo ambaye ni Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban

Na Issa Mwadangala.

Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Songwe (TPF NET) umefanya dua maalum ya kuwaombea na kuwarehemu askari wa kike waliotangulia mbele ya haki.

Dua hiyo iliyofanyika Septemba 06, 2025 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Mtandao huo ambaye ni Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban kwa unyenyekevu mkubwa aliwaombea kwa Mwenyezi Mungu awajaalie rehma, msamaha na mapumziko ya amani marehemu hao ambao ni Staff Sajenti Asha, Koplo Leokadia, na Wp Happy, huku alieleza mchango mkubwa wa marehemu hao katika utumishi wao wa Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake Mwaminat Nyamkunga mmoja wa wanajamii walioshiriki katika dua hiyo ya kuwarehemu marehemu hao, aliongeza kwa kuendelea kuwaombea dua marehemu hao, akimuomba Mwenyezi Mungu awarehemu, awaweke mahali pema peponi na kuendelea kulilinda Jeshi la Polisi na askari waliobaki.

Naye, Bi. Mwanamvua Makalo kwa upande wake alitoa shukrani zake za dhati kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kuandaa na kuratibu dua hiyo muhimu na yenye kugusa mioyo ya wengi, ambayo imewaleta pamoja Polisi wanawake na jamii kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaenzi askari wa kike waliotangulia mbele ya haki, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano na kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mambo ya kijamii ikiwa ni pamoja na masuala ya kiusalama.

Ikumbukwe kuwa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Songwe ulifanya misa ya shukurani kwaajili ya marehemu hao Septemba 01, 2025 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Vwawa iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe ili kuendelea kujidhatiti kuwaezi marehemu hao ikiwa ni pamoja na kuwafariji wapendwa wao ili kuimarisha ustawi wa ushirikiano baina ya askari wa kike na jamii katika kuendeleza misingi ya upendo, mshikamano na maombi kwa ajili ya wote waliopo na waliotangulia mbele ya haki.
WhatsApp Image 2025-09-06 at 19.00.53_96fba66f.jpg
Mwaminat Nyamkunga mmoja wa wanajamii walioshiriki katika dua hiyo. 
WhatsApp Image 2025-09-06 at 19.09.11_99bd490a.jpg

WhatsApp Image 2025-09-06 at 19.00.46_6eac2df2.jpg
WhatsApp Image 2025-09-06 at 19.00.44_41a2f9d2.jpg

WhatsApp Image 2025-09-06 at 19.00.39_88d194fb.jpg
WhatsApp Image 2025-09-06 at 19.00.49_1fb3a2f6.jpg

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.