Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kyrgyzstan, Mhe. Zheenbek Kulubaev, wamesaini Tamko la Pamoja kuanzisha Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiyrgystan.
Tamko hilo limesainiwa tarehe 26 Septemba 2025 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Pamoja na Tamko hilo, uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili utaongozwa na Mkataba wa Vienna unaosimamia Uhusiano wa Kidiplomasia (Vienna Convention on Diplomatic Relations, 1961) na sheria nyingine za kimatiafa.
Akizungumza baada ya kusaini Tamko hilo, Mhe. Waziri Kombo aliipongeza Kyrgyzstan kwa uamuzi wake wa kufungua ubalozi jijini Addis Ababa, akisema kuwa hatua hiyo ya kimkakati itarahisisha mawasiliano ya moja kwa moja na nchi za Afrika na itaimarisha ushirikiano na Tanzania kupitia Ubalozi wake nchini Ethiopia ambapo Balozi wake pia
No comments:
Post a Comment