Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara Ndz Stephen Wasira , akizungumza na Viongozi na Wanachama wa CCM Katika Mkutano wa Ndani Uliofanyika Wilayani Kisesa Katika la Kiesa Moka wa Simiyu
Na MWANDISHI WETU
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amefichua jinsi aliyekuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina alivyojaribu kutafuta msaada wa kurudi bungeni kupitia jimbo hilo baada ya kuona hawezi kufanikiwa.
Amesema baada ya kuona njia yake kurudi bungeni baada ya miaka 20 ya kuliongoza jimbo hilo, aliwaigia simu viongozi wa juu wa Chama kutengeneza mazingira ya kutaka arudishwe.
Wasira alieleza hayo j wilayani Kisesa Mkoa wa Simiyu, alipokutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kikao cha ndani kuvunja makundi na kuwaweka pamoja wana CCM ili kuwa na nguvu ya pamoja kusaka ushindi wa mgombea urais Dk. Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge na udiwani wa mkoa huo.
“Sasa ndugu yangu Mpina baada ya kuanza mchakato wa kura za maoni na watu wanachukua ‘mafomu’ (fomu) mimi alinipigia simu…akaniambia kule Meatu yeye anataka kuchukua fomu lakini anafikiri Meatu watamwonea, akasema katibu wa Meatu ataninyima fomu.
“Nikamwambia hapana, kila mwanachama wetu akiomba fomu lazima apewe, mengine yatokanayo hayo ni mengine, lakini fomu lazima apewe na atapewa, hii ilikuwa tarehe 27 mwezi wa sita aliponipigia simu.
“Akachukua fomu halafu akajaza halafu akarudisha na kila aliyejaza alikuwa anatoa sh. 500,000, kwa hiyo na sh. 500,000 lazima alitoa maana huwezi kurudisha hivi hivi.
Alisema aliporudisha ulianza mchakato kuanzia wilaya, mkoa, sekretarieti na kamati kuu, lakini jina la Mpina halikuwa miongoni mwa wanachama saba ambao majina yao yalirejeshwa kuendelea na mchakato.
“Hakulalamika wala hakuhama CCM wakati ule maana angekuwa kweli ameichukia sana CCM angehama baada ya jina kutokuwepo, lakini alikaa mwezi mzima nadhani alikuwa anatafakari.
“Lakini nafikiri watu fulani fulani watakuwa walivuruga akili ya Mpina, wakamwambia njoo huku, tena wakamwambia ukija utakuwa rais eeh…Mpina ghafla tu, labda kama urais wenyewe Mpina na nyinyi wenzangu hamuujui. Kama kuna kazi ngumu kuipata ni urais,” alisema.
Wasira alieleza kuwa, siyo lazima ikiingia bungeni ukae milele, “sasa nyinyi ndugu zangu wa Kisesa mlikuwa na mbunge wenu amekaa hapa kwa miaka 20, sasa miaka 20 hii siinatosha.”
“Na niwaambie watu waliokaa miaka 20 sio mbunge wa Kisesa tu ambaye ameachwa, hamuwezi kuwa na Bunge jipya lakini watu ni walewale wanazeekea mule, haiwezekani,” alisema.
CCM HAINA UGOMVI NA MPINA
Makamu Mwenyekiti Wasira alisema CCM hakina ugomvi na Mpina, kwa kuwa Chama kikubwa, hakiwezi kugombana na mtu binafsi.
“CCM Chama kikubwa sana katika Afrika, wengine wanakuja kutuuliza nyinyi mnaendeleaje halafu wasikie eti Chama kinagombana na Mpina, hapana, sisi hatuna ugomvi na Mpina.
“Ndugu zake Mpina mleeni Mpina kiakili wakati atakapokuwa amekosa urais ili aendelee kuwa mtu mzuri na mwanakijiji wa Mwandoya mzuri, kazi ya kumlea itakuwa ya familia na majirani zake kwa sababu urais hawezi kupata tunajua.
“Pia hatumwambii ukikosa urudi ni hiyari yake vilevile, ila akirudi tutampokea, lakini hatumwambii lazima urudi maana si lazima awe rais anaweza kuwa mwanachama wa kawaida wa chama chake kipya, lakini ana kazi kweli maana hapa Kisesa mwanachama wa hicho chama chake kipya ni yeye mwenyewe,” alisema.
No comments:
Post a Comment