Habari za Punde

MWENYEKITI WA CCM NA RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE AHITIMISHA KAMPENI ZA UCHAGUZI KATIKA MAJIMBO MATANO YA ZANZIBAR

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Taifa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ufungaj wa Mkutano wa Kampeni wa Majimbo ya CCM Wilaya ya Kusini Unguja Mkoa wa Kusini uliyofanyika katika viwanja vya Skuli ya Ghana Jimbo la Uzini Zanzibar.
Dkt. Kikwete alihitimisha kampeni hizo katika mkutano mkubwa wa wa hadhara uliofanyikia katika uwanja wa Skuli ya Ghana jimbo la Uzini Wilaya ya Kati, Shehia ya Kiboje Mkoa wa Kusini na kuhitimisha kampeni za majimbo ya Tunguu, Chwaka na Uzini katika Wilaya ya Kati, pamoja na majimbo ya Paje na Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja.

Picha mbalimbali za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alipoongoza kuhitimisha rasmi kampeni za uchaguzi kwa majimbo matano ya Zanzibar, akiwataka wananchi wa pande zote mbili za Muungano kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29 kupiga kura kwa amani, umoja na utulivu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.