Timu yetu ya Taifa, Zanzibar Heroes imetolewa katika mashindano ya Cecafa baada ya kufungwa 2-1 na timu ya taifa ya Uganda The Cranes katika mchezo wa nusu fainali uliomalizika jioni hii.
Goli la mapema lililofungwa na Steven Bengo katika dakika ya pili ya mchezo kwa kiasi kikubwa liliwachanganya wachezaji wetu na kabla ya kukaa sawa wakajikuta wakipachikwa goli la pili kwa kujifunga wenyewe baada ya kiungo mshambuliaji Abdulihalim Humoud kuingiza mpira kimiani katika harakati za kuokoa.
Kipindi cha pili, vijana wetu waliingia na uhai pamoja na kuhaha kutafuta nafasi za kuweza kurudisha magoli hatua ambayo ilizaa matunda katika dakika ya 73 wakati Abdulghani Abdullah alipoweza kupata goli la kwanza. Licha ya jitihada za washambuliaji wetu kulisakama goli la waganda lakini hatukuweza kupapatua mpaka filimbi ya mwisho.
No comments:
Post a Comment