Habari za Punde

ZOEZI LA UPIGAJI WA KURA YA MAONI UNGUJA JUU YA MUUNDO WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura cha skuli ya Kiembesamaki, ikiwa ni zoezi la kura ya maoni ya Uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akikabidhi kitambulisho chake cha upigaji kura kwa karani wa kituo cha kupigia kura Asha Mustafa Abdalla, katika Skuli ya Msingi Kiembesamaki, wakati wa zoezi la kura ya maoni Zanzibar.
Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha akizugumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari baada ya kupiga kura yake ya maoni katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki.
Mwananchi wa Kijiji cha Kijini Makunduchi Rukia Abdalla Jani akipiga kura yake katika Kituo cha Skuli ya Kijini.
Wananchi wa kijiji cha Bwejuu wakisubiri zao yao kuingia chumba cha kupigia Kura kilioko Skuli ya Bwejuu.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Zanzibar Leo Ramadhan Makame (kushoto) akizugumza na Mkuu wa Kituo cha Upigaji Kura cha Skuli ya Paje Ayoub Haji Jecha kituoni hapo wakati zoezi la uandikishaji likiendelea kituoni hapo.

Bibi huyu akitoka kutumia haki yake ya kuchaguwa anachotaka katika Kura ya Maoni ya Muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar katika zoezi la upigaji kura katika kituo cha Skuli ya Bwejuu.
Mwananchi wa Kijini Bwejuu akipiga Kura yake ya Maoni ya Muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, katika Kituo cha Skuli ya Bwejuu.
Zoezi la Upigaji Kura katika Kituo Cha Skuli ya Bwejuu akipiga kura yake.

Wananchi wa kiembesamaki wakiwa katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Kiembesamaki wakisubiri kupiga kura yao.

Afisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akimuangalia mmoja ya Mwananchi jina lake katika daftari la wapiga kura wa kituo cha Skuli ya Kiembesamaki wakati wa kura ya maoni iliofanyika Zanzibar .
Afisa kituo cha Kupigia Kura cha Welezo akimtia wino ikiwa ni alama ya kuwa tayari ameshapiga kura yake kituoni hapo.
Wananchi wa Shehia ya Welezo wakitazama majina yao katika Kituo cha Kupigia kura cha Skuli ya Welezo. ili kupata kupiga kura ya Maoni ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar zoezi linalofanyika Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.