Habari za Punde

UZINDUZI WA UMEME WA MAJENERETA YA DHARURA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akimsikiliza Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali Mbarouk akitoa maelezo katika chumba cha kusambazia umeme wa dharura Mtoni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akitembelea maeneo yaliyowekwa Majenereta baada ya uzinduzi wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Amani Abeid Karume mwenye miwani, Kulia kwake ni Waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, kulia kwa Waziri kiongozi ni mtaalamu Philip Khalaf kushoto kwa Rais ni mtaalamu mwengine Yousef Ali Yousef wakiwa pamoja na Kaimu Meneja wa shirika la umeme Zanzibar Hassan Ali Mbarouk

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akimsikiliza mtaalamu wa ufundi wa Kampuni ya Mantrac, Philip Khalaf baada ya kuuzindua mradi wa umeme wa dharura kituo kikuu cha umeme Mtoni Zanzibar.
Viongozi wa vyama vya siasa, wageni waalikwa na wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Viongozi wa Serikali pamoja na vyama vya siasa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mwakilishi wa nchi za Norway, Uingereza na Sweden zilizoshirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukamilisha mradi huo wa umeme wa dharura Zanzibar, Tom Elesther akitoa salamu
Waziri wa Maji, Ujenzi na Nishati Mansour Yussuf Himid akitoa maelezo ya uwekaji wa mradi huu wa umeme.
Wataalamu wa Kampuni ya Mantrac ya Misri iliyofunga Majenereta hayo katika kituo cha umeme Mtoni.
Wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa umeme wa majenereta ya umeme wa dharura wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.