Habari za Punde

MGOMBEA WA ALLIANCES FOR TANZANIA FARMERS PARTY SAID SOUD SAID KUWANIA URAIS WA ZANZIBAR - MTU WA TATU KUCHUKUWA FOMU YA URAIS WA ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Zanzibar (AFP) Said Soud Said
Mgombea Urais wa Chama cha Wakulima Zanzibar Alliance For Tanzania Farmers Party Said Soud Said akishindikizwa Afisi za Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar. akiingia viwanja vya tume Maisara.
Wanachama wa Chama cha Wakulima Zanzibar wakiwa Afisi ya Tume ya Uchaguzi wakimshindikiza Mgombea wao.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wakulima Zanzibar (AFP) Said Soud Said akiwa na baadhi ya Wanachama wa chama hicho wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi akitowa maelezo ya jinsi ya muongozo wa baadhi ya fomu hizo kujaza.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande akimkabidhi fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Chama cha Wakilma Said Soud Said alipofika afisi za Tume Maisara

Mgombea Urais kupitia Chama cha Wakulima Zanzibar Alliance For Tanzania Farmers Party Zanzibar. ( AFP) Said Soud Said akitia saini ya kupokea Fomu ya Urais, akishuhudiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Khatib Mwinyichande.
Waandishi wakiwa kazini afisi ya tume ya uchaguzi kufuatilia uchukuwaji wa fomu ya Urais wa Zanzibar.
Mgombea wa Chama cha Wakulima Zanzibar ( AFP)Said Soud Said akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kuchukua Fomu ya Urais Tume ya Uchaguzi kwania kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.