Habari za Punde

MAJINA YA WAGOMBEA WA UBUNGE NA UWAKILISHI ZANZIBAR YARUDI


YAWABAKISHA WALIOCHAGULIWA NA WANACHAMA ZANZIBAR.

TAKUKURU yawakosesha wengine huko Bara

Na Mwantanga Ame, ZJMMC

HATIMAE Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeyarejesha majina ya wagombea wote walioshika namba moja katika kura za maoni kwa nafasi ya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kwa upande wa Zanzibar.

CCM kimefanya uteuzi huo juzi usiku chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kumaliza kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kuyapitia majina ya wanachama wa Chama hicho walioomba nafasi hizo katika Majimbo mbali mbali ya Unguja na Pemba.

Licha ya hapo kujitokeza lawama kwa baadhi ya wagombea kupinga matokeo ya zoezi la awali la kura ya maoni kwa baadhi yao kutoridhika na mchakato huo lakini kikao hicho kimekata mzizi wa fitina na kuyarejesha majina yote yalioshika namba moja katika kura hizo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chama Cha Mapinduzi, iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Kapteni George Mkuchika, imefahamisha kuwa kwa upande wa Zanzibar waliojitokeza kuwania nafasi hizo na kushika namba moja wameteuliwa kutetea Majimbo waliyoomba ila Jimbo moja la Mkoani mgombea wake ameenguliwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.