Habari za Punde

MSAADA WA DHARURA UNAHITAJIKA HARAKA

Karibuni tumepokea ombi kutoka Hospitali ya Mnazimmoja na Afisa wa huduma za ustawi wa jamii, Bi Salama kwamba kuna mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano kutoka Micheweni Pemba ambae ana matatizo ya ugonjwa wa macho.

Mtoto alifikishwa Hospitali ya rufaa Mnazimmoja kutoka Pemba na ametazamwa na Madaktari, Mnazimmoja na kuamua kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi kwa sababu amepata uvimbe kwenye jicho lake la kushoto - left eye tumour.

Kwa bahati mbaya familia yake haina uwezo wa kugharamia gharama za safari, matibabu pamoja na kujikimu kwa kipindi watachokuwepo Dar kwa matibabu.

Zanzibar Outreach Program baada ya kupata taaarifa hizi imewasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambao wamo katika utaratibu wa kumsaidia mtoto huyu. Hata hivyo ZOP tumeona kwamba tunalo jukumu la kusaidia familia na kwa hivyo imejitolea kuchangia Shilingi Laki mbili ukijumlisha na msaada ambao utatolewa na Wizara na kwa ujumbe huu tunakuomba ujumuike nasi katika kumchangia mtoto huyu kwa kuwasiliana na

Dr Naufal Kassim 0773047979,
Dr Kassim Faki 0777416945
Afisi za ZOP +255245500711)

BANK DETAILS

JINA LA AKAUNTI: ZANZIBAR OUTREACH PROGRAM

AKAUNTI NO. : 021108 01008

JINA LA BENKI: PEOPLES BANK OF ZANZIBAR

TAWI : MALINDI

SWIFT CODE: PBZATZTZ

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ZOP ingia kwenye tovuti zanzibaroutreach.com

Dr Naufal Kassim Mohammed
ENT, HEAD & NECK SURGEON
ZOP EXECUTIVE SECRETARY

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.