Waandaaji mdahalo waeleza sababu mgombea Urais CCM kushindwa kuhudhuria
Na Mwanajuma Abdi
MSIMAMIZI wa mdahalo wa wazi wa wagombea Urais Zanzibar na Jumuiya ya Kiraia, Abubakar Mohammed Ali amesema mgombea CCM, hakushiriki mdahalo uliofanyika jana kutokana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushirikiana na jumuia hizo kuandaa sheria namba sita ya 1995 kuruhusu kuanzishwa kwake.
Mdahalo huo ni kwa ajili ya serikali itakayoundwa baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31.
Abubakar alitoa ufafanuzi huo kabla ya kuanza mdahalo huo, katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View mjini hapa.
Mdahalo huo ulihudhuriwa na mgombea mmoja wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambapo wagombea wa vyama vyengine vitano vikiwemo vya TADEA, NCCR Mageuzi, AFP, NRA na Jahazi Asilia, hawakujitokeza kwa maelezo wanataka walipwe posho zikiwemo za usafiri.
Msimamizi huyo alisema mgombea mmoja ambaye yuko Pemba alitaka alipwe posho la shilingi 80,000 pamoja na usafiri, ambapo alisisitiza kwamba hao hawako tayari kwa nafasi ya urais wa Zanzibar.
Akijibu maswala, Maalim Seif Sharif Hamad alisema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza atazijengea uwezo wa kitaalamu asasi za kiraia katika kuandika miradi mbali mbali, kutunza kumbukumbu na fedha zao katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema asasi za kiraia zina mchango mkubwa katika hivyo ataweka Idara maalum itayosimamia jumuiya hizo pamoja na kuwapatia misaada ya kujiendesha na kuondokana na utegemezi wa wafadhili kutoka nje ya nchi.
Aidha alieleza amekusudia kuanzisha taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ili kudhibiti mapato ya serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Akizungumzia suala la watu wenye ulemavu, alifahamisha kuwa, katika CUF inakusidia kuweka takwimu za watu wenye ulemavu wa aina tofauti ili kuweza kuwapatia mahitaji yao ikiwemo elimu, huduma za afya, kujenga majengo yatayowarahisishia kufika na kuwachagua katika nafasi za maamuzi .
Mgombea huyo, alieleza amekusudia kuviunganisha vyombo vya habari vya Serikali ikiwemo Televisheni Zanzibar na Sauti ya Tanzania Zanzibar kwa kuligeuza kuwa Shirika la Utangazaji la Zanzibar, ambalo litaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kama TBC

@Mapara,
ReplyDeleteHii stori haifahamishi vizuri kwanini mgombea wa CCM hajahudhuria mdahalo, ukisoma vizuri huo ufafanuzi unautata mtupu, nanukuu," mgombea CCM, hakushiriki mdahalo uliofanyika jana kutokana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushirikiana na jumuia hizo kuandaa sheria namba sita ya 1995 kuruhusu kuanzishwa kwake".
Mimi sijafahamu hapa waliofahamu wanambie hiyo nukuu inamaanisha nini?
Mdau Misri
Hii nimeitoa katika gazeti la Nipashe
ReplyDeleteNaibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa NCCR- Mageuzi, Nadir Joseph Nyoni, alithibitisha chama chake kupokea mwaliko huo.
Hata hivyo alisema mgombea wa chama hicho, Haji Hassan Khamis hakuweza kushiriki kutokana na matatizo ya kifamilia.
"Tulipata mualiko lakini mgombea wetu amepata msiba na amesafiri kwenda Pemba", alisema Nyoni.
Mgombea kupitia AFP, Said Soud Said, alisema chama chake kimeshindwa kushiriki katika mdahalo huo kwa sababu hauna maslahi ya kifedha.
"Hatuwezi kushiriki kwa sababu hatupewi pesa na waandaaji, wakati wao wanalipwa", alisema Said.
Viongozi wa CCM hawakuweza kutoa maelezo mara moja juu ya kutoshiriki katika mdahalo huo. Lakini wiki iliyopita akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti, Katibu Mkuu wa CCM Yussuf Makamba alisema chama chake hakitawaruhusu wagombea wao kushiriki midahalo.
Alisema hatua hiyo ilifikiwa kwa sababu fursa ya kuulizwa maswali na kutangaza sera zao wanaipata kwenye mikutano ya kampeni
Mbali na kusoma muhtasari wa yaliyojiri katika mdahalo huu, ninadhani taaluma ya kublogu na uripoti habari inayo mengi ya kujifunza kutoka kwa jamaa wa Zanzibar.
ReplyDeleteNimevutiwa sana na uripoti wa Othman Maulid Othman kutokana na alivyoweza kuchukua picha za matukio tofauti na kuweza kumpa msomaji ambaye hakupata fursa ya kuhudhuria au kutizama mdahalo huo, kuweza kupata picha kamili ya ilivyokuwa ukumbini humo. Ameweza kuchukua picha ya mmoja wa waliodahiliwa, amechukua picha ya kundi la Waangalizi wa nje ya nchi, amechukua kundi la Wawakilishi wa vyama vya kiraia (AZAKI), zaidi sana, amechukua picha ya kundi la Walemavu ambao mara nyingi, aidha husahauliwa kabisa katika shughuli mbalimbali ambazo zinawagusa wachilia mbali kutokuthaminiwa.
Aina hii ya uandishi na uripoti habari inastahili kusifiwa na kupongezwa. Huu ni mmojawapo ya mifano mizuri kabisa ya kuigwa.
Ninampongeza kwa dhati kabisa Othman Maulid Othman kwa hili.
credit source: http://www.wavuti.com/4/previous/6.html#ixzz10wDGOt4P