Na Mohamed Gharib,
Wananchi wa Mkoa wa Mjini/Magharibi wamepongeza huduma nzuri zinazotolewa na gari za abiria maarufu daladala jinsi zinavyohudumia abiria kwenye mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi Ndugu Maryam Ali Kombo wa Kibweni amesema kuwa amefurahishwa namna utaratibu mzuri uliopo wa kuziongeza gari za daladala katika kutoa huduma bila ya usumbufu.
"Umeona pale daladala zilivyojaa tofauti na Ramadhani wa mwaka jana ilikuwa saa kama hizi hupati usafiri bila ya kutia kibega", akimuonesha kwa kidole mwandishi wa habari hizi eneo la stendi ya Darajani lilivyoshehena gari za daladala.
Alitoa mfano wa njia ya Bububu hivi sasa ina gari nyingi. Alizitaja njia zenyewe ni Bububu/Mnazimmoja, Bububu/Uwanja wa Ndege, Bububu/Fuoni na Kijichi/Darajani. Hii ni ishara kuwa sasa mji wetu wa Unguja umekua kibiashara na kimiundo mbinu.
Safia Ali Makame mkaazi wa Fuoni alisema kuwa usafiri wa safari hii ni mfano mzuri wa kuigwa kwa Wilaya na Mikoa yote ya Zanzibar.
Tunashukuru gari zimeongezeka na njia zimekuwa nyingi kiasi kwamba si lazima siku hizi kupitia Darajani kama unataka kwenda sehemu nyengine ya mji wa Unguja. Kitu pekee kinachosumbua ni abiria kujazwa kupita kiwango kilichoruhusiwa daladala kuchukua abiria.
Mfano alitoa gari ya abiria 16 utakuta inachukua abiria hata 25 bila ya kujali wazee au watoto wadogo.
Hivyo ameshauri mamlaka zinazosimamia daladala likiwemo jeshi la Polisi la Usalama Barabarani kusimamia ipasavyo daladala zinazozidisha abiria kupita kiwango kilichopangiwa.
Naye dereva wa njia ya Fuoni Ndugu Khamis Hamad Saleh amesema kuwa wanapata taabu wanapopita na gari zao katika eneo la soko la Mwanakwerekwe kwa sababu ya msongamano wa magari na wananchi wanaokuja kutafuta mahitaji mbali mbali sokoni kutokana na barabara ya sehemu hiyo kuwa ni nyembamba.
Huu msongamano unasababisha foleni kubwa na hata saa nyengine misafara ya viongozi wa kitaifa wanapopita hutokea mtafuruku ambao ni hatari kwa usalama wa viongozi hao.
Hivyo ameshauri Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi na Baraza la Manispaa kulipanua eneo hilo kwa kujenga barabara pana na kutenga sehemu maalum ya kuzihifadhi gari zinazofika hapo sokoni.
Hata hivyo ameshukuru kuona ongezeko la abiria katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani licha ya gari kuongezeka.
Hivyo ameshauri mamlaka zinazosimamia uendelezaji wa usafiri kwa Mkoa wa Mjini/Magharibi kuwawezesha ili kwenda na sayansi na teknojia mpya ya usafirishaji abiria kwa kuweka vituo vya abiria ili kuweza kupata huduma muhimu pale kituo kikuu cha Darajani kwa kutia taa za mwanga mkali, vyoo vya kisasa na mabanda ya kupumzikia abiria wakati wa mvua au jua kali.
Ndugu Khamis amesema abiria wengi wanapotoka safarini kama vile Pemba au Dar es Salaam na wanafunzi wa skuli mbali mbali hupata taabu ya kupata sehemu ya kupumzikia kutokana na jua kali liliopo hapo wakati wa mchana.

No comments:
Post a Comment