Asema Bandari ya Mkoani kujengwa upya
Miundombinu, huduma za jamii kuimarishwa zaidi
Na Bakari Mussa, Pemba
MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema endapo atapewa ridhaa ya kuiongoza Zanzibar hatowavumilia wale wenye lengo la kuichezea amani na utulivu uliopo.
Alisema Wanzanzibari wanapaswa kuringia amani na utulivu uliopo kwani ndio msingi wa kujiletea maendeleo na hatokubaliana na mtu yeyote atakayejaribu kuichezea amani.
Mgombea huyo wa CCM, alisema hayo jana huko Chokocho, Mkoa wa Kusini Pemba wakati akiendelea na kampeni zake za kuwania kiti cha Urais wa Zanzibar.
Alisema amani iliyopo inaweza kuendelezwa na Chama kimoja tu nacho ni CCM na kuwataka wananchi kukipigia kura ili kiweze kuiendeleza sera hiyo.
Dk. Shein aliwataka CCM wananchi kukichagua chama hichi kwani sera zake zina lengo la kuinua na kuboresha maisha ya wananchi.
Akizungumzia sekta ya jamii alisema, endapo atapewa ridhaa ataimarisha miundombinu ya maji safi na kuwapatia wananchi huduma hiyo kutoka asilimia 70 ya sasa hadi 95 kwa wakaazi wa mjini, huku pia akiazimia kuboresha huduma hiyo kutoka asilimia 60 hadi 80 kwa wananchi wa vijijini.
Kuhusu nishati ya umeme, Dk. Shein alisema serikali mpya ya CCM itahahakikisha inafikisha huduma za umeme kwenye visiwa vidogo vidogo vikiwemo Kisiwa Panza, Shamiani Muambe na Makoongwe.
Aidha alisema atajenga skuli 21 mpya za kisasa katika maeneo mbali mbali ya Mkoa huo ili kuwaondoshea shida ya masomo watoto.
Kuhusu sekta ya Afya alisema ataipandisha hadhi hospitali ya Abdulla Mzee iliyopo Mkoani na kuwa hospitali ya mkoa sambamba na kujengwa vituo vya afya kwenye maeneo ambayo hayana vituo hivyo.
Akizungumzia kuhusu bandari ya Mkoani alisema bandari hiyo itajengwa upya sambamba na kuwekewa vifaa vipya kwa ajili ya upakiaji na upakuzi wa mizigo.
Mgombea huyo alisema CCM ina uhakika wa kushinda kwenye uchaguzi huo ikitegemea kupendwa na watu wengi sambamba na uzito wa sera zake.
Dk. Shein aliwataka wananchi wa kukipigia kura chama hicho kwani sera zake zinatekelezeka na zimekuwa zikiwafikia wananchi wote.

No comments:
Post a Comment