Habari za Punde

UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM, KIBANDA MAITI

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM na Makamo wa Rais wa Tanzania Dk Ali Mohammed Shein akizindua Ilani ya CCM katika uzinduzi wa Kampeni leo.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,akimkabidhi Ilani ya ya Chama cha Mapinduzi,Mgombea Urais wa Zanzibar,na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohammed Shein, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti Mjini Unguja
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,akiteta jambo na mgombea Urais wa Zanzibar kwa upande wa CCM Dk Ali Mohammed Shein,wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti Mjini Unguja.



Wananchi na wanachama wa CCM Zanzibar wakiwa katika uzinduzi wa Mkutano wa kampeni za CCM huko viwanja vya Kibandamaiti Mjini Unguja jana.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal akisalimia na Mama Fatma Karume alipowasili viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Urais wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.