Wanahabari msiwe chanzo cha vurugu - UDP
Masanja Mabula, Pemba
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Zanzibar, Juma Khamis Faki, amewataka waandishi wa habari na vyombo vya ulinzi kutokuwa chanzo cha kuchafuka amani na utulivu uliopo huku taifa likielekea kwenye uchaguzi Mkuu.
Naibu huyo alisema hayo jana katika viwanja vya Shamiani Chakechake Pemba kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho.
Alisema waandishi wana jukumu la kuienga enga amani iliyopo kwa kuepuka kutumiwa na wanasiasa wanaopenda madaraka kwa njia ya mkato na kuchafua wenzao.
Katibu huyo alisema waandishi wanaweza kuepukana na lawama hizo endapo wataandika ukweli bila ya kutumiwa kumchafua mtu, kumpendelea au kuandika uchochezi.
Faki aliwanyooshea vidole baadhi ya wanasiasa akisema wamekuwa na tabia ya kukumbatia vyombo vya habari ambapo badala ya kuvieleza yale yenye maslahi ya umma hutaka waandikwe mambo yao binafsi.
"Huu ni wakati mbaya sana kwa waandishi wa habari watajitokeza wanasiasa uchwara kutaka wakutumieni na kukudanganyeni kwa vijisenti, lakini msikubali tumieni taaluma yenu kuandika ya ukweli", alisema.
Akizungumzia vyombo vya Ulinzi, Katibu huyo alisema vyombo hivyo vinajukumu la kulinda amani kuanzia wakati wa kampeni hadi uchaguzi mkuu, hivyo ni wajibu wao kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wanasiasa ambao watakwenda kinyume sheria.
Alisema wapo viongozi wanaopenda kusababisha chokochoko hasa katika kipindi kama hichi ili kuliweka taifa kwenye hali ya taharuki huku akitaka wanasiasa wa aina hiyo wadhibitiwe.
Katibu huyo mbali ya kuzindua kampeni za chama hicho pia alitumia fursa hiyo kuwatambulisha na kuwaombea kura wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

No comments:
Post a Comment