Habari za Punde

CHANEZA YASEMA RAIS KIKWETE ATACHAGUWA WAZIRI MWENYE UCHUNGU NA MICHEZO

Na Mwajuma Juma

CHAMA Cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA), kimesema kuwa wanaimani kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete atachaguwa Waziri wa Michezo mwenye uchungu wa michezo na atakaewaunganisha Watanzania katika michezo.

Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Rahima Bakari kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari inayompongeza Rais Kikwete kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa hiyo ya Novemba 10 mwaka huu, imesema kuwa wanaamini ushindi alioupata Rais Kikwete ni ushindi tosha unaokubalika katika utendaji wake wa kazi, katika kuhudumia Wananchi wake.

"Uongozi wa CHANEZA tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Kikwete kwa kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", ilieleza Taarifa hiyo na kuongeza "Ni imani yetu kwamba safari hii Mheshimiwa Rais atatuchagulia Waziri wa Michezo asiyependa majungu na mfarakano na atakaeweza kuunganisha Watanzania katika nyanja za michezo", ilieleza taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.