Habari za Punde

DK SHEIN AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA DODOMA

Rajab Mkasaba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amehudhuria sherehe za kumuapisha Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Sherehe hizo za kumuapisha Waziri Mkuu Pinda zilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mgeni Rasmi katika hafla hiyo.

Viongozi mbali mbali wa vyama na serikali, Mabalozi na wageni wengine waalikwa walihudhuria katika sherehe hiyo akiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd.

Rais Kikwete alimteua Mhe.Pinda kuendelea kushika wadhifa wake huo.Tangazo la rasmi lilitoka rasmi kwa jina la Pinda kuwasilishwa mbele ya Wabunge kwenye kikao maalum cha Bunge na kauli moja wabunge wakathibitisha uteuzi huo bada ya kuhojiwa na Mwanasheria mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kisha likafuata zoezi la kupiga kura ambazpo idadi ya kura zote zilizopigwa zilikuwa 328.

Kati ya kura hizo Pinda alipata kura za ndio 277 sawa na asilimia 84.5, kura za hapana zilikuwa 49 sawa na asilimia 14.9 kura zilizoharibika zilikuwa 2 sawa na asilimia 0.6.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.