Hivi karibuni tumeshuhudia maendeleo ya uteuzi wa baadhi ya Waheshimiwa ambao wamegombea ima uwakilishi au ubunge katika majimbo yao na kushinda na kisha kuteuliwa kama ni Wabunge au Wawakilishi na Rais mhusika.
Kitendo hiki ambacho kimetokea kwa Makamo wa pili wa Rais, Balozi Iddi Seif ambae alipita bila ya kupingwa katika kinyan’ganyiro cha ubunge katika jimbo la Kitope na kisha kuteuliwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein kama mwakilishi wa kuteuliwa akitumia uwezo aliopewa na Katiba ya Zanzibar kuteua wajumbe kumi.
Pia kinamhusisha Waziri Kiongozi Mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha ambae alishinda kiti cha uwakilishi katika jimbo la Mwanakwerekwe na kisha kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete kama ni Mbunge wa kuteuliwa nae pia akitumia uwezo wa kikatiba.
Matukio haya mawili tukiyachukulia katika mtazamo wa mpiga kura ni kwamba yule waliomchagua kuwawakilisha katika chombo cha kutunga Sheria iwe ni Bunge au Baraza la Wawakilishi atashindwa kuwajibika ipasavyo kwa kuvaa kofia mbili ambazo utekelezaji wake utakuwa mgumu. Kwa maana nyengine watakosa mwakilishi katika moja ya mihimili hii miwili muhimu. Mara nyingi vikao vya Bunge na Uwakilishi huwa katika wakati unaofanana sasa sijui itawezekana vipi kuweza kuwepo Dodoma na Chukwani kwa wakati mmoja wakati mpiga kura akitegemea shida zake atakazozifikisha kwa Mbunge wake aliyeteuliwa Mwakilishi au Mwakilishi wake alieteuliwa Mbunge kushindwa kufikishwa katika vyombo husika vys kutunga sheria.
Sijui wadau mnalionaje suala hili
kwa kweli kwa upande wangu mimi naona wafikirie tena, kwa utekelezaji wa kazi utakuwa pungufu na haki za wananchi zitapotea iwapo watakuwa na shida za kufuatiliwa kwa waliowachagua.
ReplyDeletetatizo ni mfumo wa muungano nao pia unachangia, hhizi serikali mbili zilokuwepo haizeleweki, kwann tusikae chini tukafumua kila kitu na kuweka mambo sawa? mfumo mzur utakaogawanya majukum vizur ni kuwa na serikali 3
ReplyDelete