Habari za Punde

UZINDUZI WA CHAMA CHA MCHEZO WA PIKIPIKI ZANZIBAR ZAMOCA KIWANJA CHA KISONGE.I

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Said Shaaban akizinduwa Chama cha Mchezo wa Pikipiki Zanzibar katika Viwanja vya Kisonge Michezani.
WAPANDA Pikipiki wakikaguwa Njia watakayopika kwa maonesho ya Mchezo wa PIKIPIKI 
VIONGOZI wa WEizara yaHabari Utamaduni na Michezo na Wafadhili wa Mchezo huo wakisimama kwa Dakika moja kumuombea muanzilishi wa Chama hicho Salum Khatib Bogoyo kabla ya Uzinduzi wa Chama hicho Kiwanja cha Kisonge Michezani.
WANAMICHEZO wa Mchezo wa Pikipiki Zanzibar wakijiandaa kwa kuonesho mchezo huo katika kiwanja cha Kisonge Michezani.
MOJA ya njia zinazopita pikipiki iliotengenezwa kwa ajili ya maonesho hayo kiwanja cha Kisonge Michezani.
WANAMICHEZO wa Mchezo wa Pikipiki wakipita katika Tuta maalum lilolowekwa kwa ajili ya kupitia pikipiki kiwanjani hapo.
WAPANDA Pikipiki katika mchezo wa uzinduzi wa Chama Chao cha MCHEZO wakionesha maonesho ya mchezo wa kurusha mapikipiki kwa Wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi huo.  
WANANCHI waliofika kuangalia uzinduzi wa Chama cha Mchezo wa Pikipiki ZANZIBAR, wakifuatilia mchezo huo uliofanyika kiwanja cha Kisonge Michezani na kuwashirikisha Mafundi wa Pikipiki wa Gereji za Rahaleo kwa Bogoyo.  

ABDUL Salum Bogoyo ambaye ni mtoto wa marehemu Bogoyo akiwa ni moja wa wanamichezo wa mchezo wa kurusha pikipiki uliozinduzliwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo Zanzibar Said Shaaban katika Kiwanja cha Kisonge MICHEZANI. 
 Mwanamichezo ya Pikipiki Yussuf Abdi akionesha umahiri wake wa kurusha pikipiki uliofanyika kiwanja cha Kisonge.
MPANDA Pikipiki akionesha umahiri wake wa kurusha pikipiki katika moja ya mchezo wa uzinduzi wa chama chao cha Michezo ya Pikipiki Zanzibar.

WAZAZI wa Vijana Wapanda Pikipiki wakiwa katika sare ya Chama hicho wakiwaunga mkono watoto wao katika uzinduzi wa Chama cha uliofanyika kiwanja cha Kisonge Michezani.Wakiongozwa na Bi. Mtembezi Bogoyo katikati mwenye miwani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.