Habari za Punde

WANAFUNZI PEMBA WAASWA KUTHAMINI ELIMU.

Na Bakar Mussa, Pemba

WANAFUNZI kisiwani Pemba, wametakiwa kuthamini suala zima la elimu kwa vile ndio mkombozi mkuu wa maisha yao ya baadae katika kujipatia maendeleo ya haraka na kuweza kupambana na umaskini.

Akizungumza na wanafunzi na wanachama wa maktaba katika kituo cha American Corner huko Chake Chake, Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohed Idd Juma, alisema wanafunzi wanapaswa kuzitumia fursa zilizopo nchini iliwawezez kujitafutia elimu pahala popote pale.

Alisema kwa sasa milango iko wazi kwa mtu yeyote mabae ana hamu ya kusoma hata akiwa mzee kewani fursa za kujiendeleza zipo nje na ndani ya nchi na serikali iko pamoja nao kwa hilo kwa vile inahitaji wataalamu wa fani mbali mbali.

Aliwasisitiza wanafunzi kujitahidi katika masuala ya elimu kwani bado wakati wanao wa kutosha wa kushughulikia na wasikubali na wakatae kabisa kujiingiza katika mambo ambayo yataathiri maendeleo yao ya kielimu.

Afisa huyo aliwataka wanafunzi hao kukitumia kituo hicho cha American Corner kwa ajili ya kujipatia elimu sambamba na maktaba iliopo Chake Chake Pemba, kwani ndio sehemu pekee ya kufanyia mazoezi ya masomo ili waweze kufanya vyema katika mitihani yao inapofika.

Alisema ni vyema wanafunzi wakajenga utamaduni wa kutembeleana kutoka skuli moja kwenda nyengine kwa nia ya kubadilishana mawazo ya kimasomo.

Nae Mkuu wa Kituo cha Americana Corner Pemba, Mohamed Ali, alisema kuwa Wiki ya Elimu Kimataifa huazimishwa kila mwaka Novemba 15-19 , hivyo Zanzibar ikiwa nimiongoni mwa mataifa na mwanachama wa Vituo vya American Corner haina budi kuungana na wenzao kusherehekea siku hiyo muhimu kwao.

Alisema lengo la kuadhimisha wili hiyo , ni kutilia mkazo na kuimarisha mipango thabiti ya elimu kitaifa na kimataifana ambapo kwa kawaida watu hutoka taifa moja kwenda taifa jengine kwa ajili ya kujifunza.

Alieleza elimu ni miongoni mwa mambo yanoyoimarisha soko la ajira na kukuza uchumi wa nchi , sekta ambayo imeweza kuiletea Marekani zaidi ya dola bilioni 17.7 kati ya mwaka 2008/09.

Alifahamisha kuwa kwa vile kiingereza ni kikwazo kikubwa katika kufikia elimu ya kimataifa, kituo chs American Corner Pemba, kitakuwa kinaandaa mashindano ya kiingereza kwa lengo la kuwaunganisha watoto kimasomo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.