Habari za Punde

NAHODHA, PROFESA MNYAA NA MEGHJI WATEULIWA NA KIKWETE KUWA WABUNGE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wabunge watatu (3) kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Ikumbukwe kwamba wote hawa wana asili ya Zanzibar wakati Shamsi Vuai Nahodha alikuwa Waziri  Kiongozi katika Serikali iliyopita, Profesa Makame Mnyaa ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Tswhane University of Technology, Pretoria, South Africa.m Bi Zakia Meghji ni mmoja katika Mawaziri wakongwe kwani alikuwa katika baraza la Mawaziri enzi za Mkapa pamoja na Kikwete. 
Kwa mwelekeo wa upepo unavyoelekea inawezekana kuwemo katika Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Muungano. Tusubiri tuone. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.