Timu ya Taifa ya Zanzibar – Zanzibar Heroes inaingia tena kibaruani leo kwa kupambana na timu ngumu ya Ivory Coast katika kinyan’ganyiro cha kugombania kombe la CeCafa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
Timu alikwa ya Ivory Coast inaundwa na vijana chipukizi ambao wote wanacheza soka katika nchi yao hivyo haina wachezaji wa kuklipwa.
Kocha wa Zanzibar Heroes, Stewart Hall kutoka Uingereza amewaambia wachezaji wake wasitishike na majina huku nahodha Nadir Haroub Cannavaro akiwaeleza wenzake wasiwe na hofu lakini akawataka Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono kwani hakuna kiingilio katika mchezo huu.
Tuiombee dua timu yetu ifanye vyema na kuweza kuwafunga Ivory Coast na hivyo kujihakikishia kuingia raundi ya pili ya mtanange huu.
YES YOU CAN DO IT
No comments:
Post a Comment