Leo ni tarehe 09 Muharram 1432 15/12/2010 ni Taasua na kesho ni tarehe 10 Muharram 1432 16/12/2010 ni Aashuuraa.
Ni Sunnah kufunga katika siku hizi kutokana na hadithi ya Mtume Swalla Allaahu 'Alayhi Wasallam kwamba Mwenye kufunga siku ya Aashuuraa husamehewa madhambi ya mwaka uliopita. Muslim
Kufunga siku ya Taasua ni kutokana kauli ya Mtume Swalla Allahu 'Alayhi Wasallam kwamba tutofautiane na Mayahudi kwani Mayahudi pia hufunga siku hii wakisherehekea kuokolewa kwa Mtume Musa 'Alayhi Salaam. Nae Mtume Swalla Allahu 'Alayhi Wasallam alisema kama Allah atamuweka hadi mwaka ujao angelifunga na siku ya tisa - Taasua.
Shime Waumini tujitahidi kufunga katika siku hizi mbili. Tunajaribu kuwakumbusha ndugu zetu Waislamu ikiwa leo hujawahi basi jitahidi kesho InshaAllah uwe miongoni mwa watakaofunga.
No comments:
Post a Comment