Na Mwanajuma Abdi
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema mradi wa upangaji miji (master planning) wa mjini na vitongoji vyake utakaogharimu dola za Marekani milioni 2.2, unakusudiwa kuanza mwakani Zanzibar.
Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Mwalim Ali Mwalim amesema mradi huo utaanza mwakani mjini na vitongoji vyake.
Alisema mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Aga Khan Trust of Culture, ambapo upangaji huo utazingatia hali ya mji ulivyo kutokana na msongamano mkubwa wa magari ulivyo kwa sasa.
Alieleza zoezi hilo litasaidia kufanyika kwa tathmini ya matumizi mazuri ya rasilimani zilizowepo nchini.
Alifahamisha kuwa, upangaji huo pia utazingatia kuwepo kwa maeneo ya wazi, viwanja vya michezo, huduma za jamii hospitali, maduka, barabara na nyumba za makaazi, ambazo zitazokuwa na nafasi ya kuwepo kwa maegesho ya vyombo vya moto.
Mwalim alisema maandalizi ya mradi huo yameanza, ambapo kazi ya kumpata mshauri wa kufanya kazi hiyo inakusudiwa kufanyika Aprili mwakani.
Alifafanua kuwa, zoezi hilo litakapoanza kunaweza baadhi ya nyumba zinaweza kubomolewa ili mji uweze kupangika vizuri.
Alitoa mfano nyumba za Maendeleo Michenzani na jengo la Benki ya BOT zimejengwa vizuri, ambapo kumeweza kupatikana maeneo ya maegesho ya magari, hivyo mji lazima uendane na mazingira hayo ili uweze kuvutia kama mji mengine duniani
No comments:
Post a Comment