Habari za Punde

PICHA YA BAADHI YA VIFAA VINAVYOTARAJIWA KUTUMWA KUTOKA SEATTLE, USA KWENDA ZANZIBAR




Picha za  baadhi ya vifaa tunavyotarajia kuvituma mwezi Januari 2011 na pia kuonesha makusudio suala hili lipo kwa ajili ya kutoa changamoto kwa ndugu zetu kusaidia juhudi ya kuchangia fedha usafirishaji kutoka hapa Seattle hadi Zanzibar mwezi Jan 2011 kwa hiyo wote ambao wanaweza kuona picha na vifaa vyenyewe wanaweza kutoa maoni yao , nina imani huko nyumbani Tanzania kuna matatizo ya aina nyingi yakiwemo huduma za vifaa vya maktaba na shule zetu tumia nafasi yako kama raia wa Tanzania na Zanzibar kutoa mchango wako wa kifedha kuondoa vifaa vyote na kutoa zawadi kwa wananchi wenzetu waliopo huko Tanzania katika kuboresha huduma za Elimu na maendeleo ya jamii ya Mtanzania

Zingatia Barua huko nyuma zilizotumwa online kuhusu masuala ya kutoa mchango katika account mbali mbali hapa Seattle tunawaomba wote waliopokea huko nyuma kutizama na kutumia fursa hii katika kutoa michango yao ya hiyari ambayo ni muhimu sana katika kuhakikisha vifaa vyote vinaweza kupata njia ya usafirishwaji

Natarajia mashirikiano mema kutoka kwa watanzania wote , nipo tayari kutuma kwa mara nyengine barua za michango katika email zenu.



Ahsante sana


Amin Ally 

3 comments:

  1. MZEE OTHMAN CHEI CHEI EBOU HAPA NILIKUWA NA SEMAJE, MBONA HUJAWEKA INFORMATION ZOZOTE ZA HUKO SEATTLE KAMA KUTAKUWA NA WAHISANI WAWEZE KUSAIDIA JAPO MCHANGO WA KIFETHA. HABARI HII NAWATAMBULISHA WATANZANIA WALIOPO WASHINGTON DC PIA WATAIYONA. SHKRAN. MAONI KUTOKA KWA EBOU SWAHILIVILLA.BLOGSPOT.COM

    ReplyDelete
  2. Chei chei labda ulikuwa hufuatilii hii habari n ya muda sasa na taarifa zake zpo hapa http://othmanmapara.blogspot.com/2010/12/ombi-la-michango-kusaidia-usafirishaji.html

    Ahsnate

    ReplyDelete
  3. Asante sana kaka othmani sasa nitafuatilia vilivyo shkuran.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.