Habari za Punde

UGENI WA DR. ABU AMEENAH BILAL PHILIPS NCHINI TANZANIA


Assalaamu 'Alaykum Warahmatullaahi Wabarakaatuh

Dr. Bilal Philips (Dr. Abu Ameenah Bilal Philips) mzaliwa wa Jamaica na raia wa Canada atawasili Dar es Salaam, Tanzania, Ijumaa ya Desemba 17, 2010. Dr. Bilal Philips alikuwa Mkristo na mwaka 1972 alisilimu na kuwa Muislamu. Dr. Bilal ni msomi mashuhuri duniani wa ngazi ya PhD, aliyoipata Chuo Kikuu cha Wales, Uingereza. Shahada yake ya kwanza (B.A) ya fani ya Elimu ya Dini ya Kiislamu aliipata Chuo Kikuu cha Madina.

Dr. Bilal amealikwa na Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wataalam wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO). Madhumuni ya ziara ya Dr. Bilal ni kufanya kazi ya Daw’ah kuanzia Desemba, 17 mpaka 24, 2010, katika jiji la Dar es Salaam, Morogoro mjini na Zanzibar (Unguja). Katika kazi hiyo ya daw’ah atafanya muhadhara siku ya Jumamosi, Desemba 18, 2010, kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana, katika ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia, Dr. Bilal atafanya muhadhara Siku ya Jumapili, Desemba 19, 2010, saa 2.00 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana, katika ukumbi wa Diamond Jublee, Dar es Salaa. Siku ya Jumatatu, Desemba 20, 2010, saa 10.00 asubuhi mpaka saa 6.30 mchana, Dr. Bilal atafanya muhadhara Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro. Akiwa Morogoro, Dr. Bilal atatembelea miradi ya The Islamic Foundation ambayo ni pamoja na Redio Iiman, Kituo cha Yatima na Shule ya Dar Alqam.

Siku ya Jumanne, Dr. Blala atarejea Dar es Salaam na kutembelea Ofisi ya Muft wa Tanzania, Sheikh Issa bin Shaban Simba, Ofisi ya Sheikh Musa Kundecha, Sheikh wa Baraza Kuu. Siku hiyo hiyo ya Juamanne, kuanzia saa 8.00 chana, Dr. Bilal ataanza kuendesha semina kwa watu wanaofanya kazi ya Daw’ah, kutoka Bara na Visiwani, katika moja ya shule za Kiislamu. Jumatano, Desemba 22, 2010, kuanzia saa 1.00 asubuhi mpaka 6.00 mchana, Dr. Bilal ataendelea na semina.

Jioni ya Jumatano hiyo hiyo atakwenda Zanzibar ambapo atafanya mihadhara miwili. Muhadhara wa kwanza ni Alhamisi, Desembna 23, 2010, kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana, katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Chukwani. Mchana wa siku hiyo hiyo atatembelea Ofisi ya Muft wa Zanzibar, Redio Nuur na Shule inayomilikiwa na UKUEM. Jioni ya Alhamisi, Dr. Bilal atafanya muhadhara wa pili, kuanzia saa 10.30 mpaka 12.oo jioni, katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Zanzibar (SUZA). Dr. Nbilal atakuja na mke wake ambae nae alisimu, Dada Sara.

Ziara yote ya Dr. Bilal itarushwa hewani live na kituo cha Redio Iiman cha mjini Morogoro, kinachomilikiwa na The Islamic Foundation. Pia ziaran hiyo itarikodiwa na kuzaliwa DVD, CD, n.k. – insha Allah. Waislamu na Wasiokuwa Waislamu, wote mnakaribishwa katika mihadhara iliyoelezwa hapo juu.

Wassalaamu Alaykum, Sharifu Muhammed, Mratibu wa Ziara ya Dr. Bilal. Mawasiliano zaidi piga: 0716-776226, , 0655-003744, 0655-654900, 0767-127718, 0754-208585

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.