Habari za Punde

ALIYERUHUSU WACHEZAJI 12 ATOZWA FAINI ELFU KUMI!

Na Salum Vuai, Maelezo

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) Wilaya ya Mjini, kimemtwanga faini ya shilingi elfu kumi pamoja na kumpa onyo kali muamuzi aliyechezesha mechi ya ligi daraja la pili huku timu moja ikiwa na wachezaji 12 uwanjani.

Muamuzi huyo Abdulrahman Mahfoudh alikuwa akipuliza firimbi katika mechi iliyozikutanisha timu za Muembebeni na Mkunguni hivi karibuni kwenye uwanja wa Amani B, ambapo Muembebeni ilikuwa na wachezaji 12 uwanjani huku muamuzi huyo akiwa hana habari.

Aidha muamuzi huyo alishindwa rufaa kanuni za mchezo kwani alichezesha pambano hilo kwa muda wa dakika 80 tu badala ya 90 kama sheria za FIFA zinavyoelekeza, huku Mkunguni ikiwa nyuma kwa goli 1-0.

Kutokana na kasoro hizo, timu ya Mkunguni iliamua kukata rufaa ZFA Wilaya ya Mjini kutaka haki itendeke.

Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Hassan Haji Hamza, ameliambia gazeti hili kuwa mbali na hukumu hiyo, mchezo huo pia umeamuliwa urejewe katika tarehe itakayopangwa baadae.

Hata hivyo, alisema chama chake kimetoa hukumu hiyo hafifu kutokana na kukabiliwa na uhaba wa waamuzi katika ligi zake, hivyo, kimeona ni vyema kisimfungie muamuzi huyo

3 comments:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. matusi si mazuri changia au toa Maoni

    ReplyDelete
  3. Na kama hana maoni akae kimya hapataharibika kitu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.