Habari za Punde

UZINDUZI WA SKULI MPYA YA KISASA BOPWE - PEMBA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein, akikata utepe na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe, Alfonso  Lenhardt, kuashiria uzinduzi wa Skuli ya Sekondari ya Bopwe,wilaya ya Wete kaskazini Pemba jana.
 Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt  akiwapongeza wasoma utenzi  Zuhura Khamis na  Samira Bakari, walipohani utenzi wao wakati wa sherehe za uzinduzi wa Skuli Mpya ya kisasa ya Bopwe,wilaya ya wete,Jimbo la Gando jana
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohammed Shein,akizungumza na wazee na wanafunzi na wananchi wa Jimbo la Gando,wakati wa sherehe za uzinduzi wa Skuli mpya ya kisasa ya Bopwe, Jimbo la Gando, wilaya ya Wete jana, iliyojenga kwa Msaada wa Serikali ya Marekani na Serikali ya mapinduzi Zanzibar.
 Mwalimu  Viwe Omar Sharif  akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,na Balozi wa Marekani Nchini  Alfonso Lenhardt, walipotembelea darasa la wanafunzi baada ya ufunguzi rasmi wa Skuli ya Bopwe jimbo la Gando jana.

Baadhi ya wanafunzi wa Skuli mbali mbali za  Jimbo la Gando Wilaya ya Wete wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Skuli Mpya ya Kisasa ya Bopwe, iliyojengwa kwa msaada wa  Serikali ya Marekani,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alipokuwa akizungumza  na wananchi baada ya Uzinduzi rasmi jana.

Picha na Ramadhan Othman, Wete Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.