Habari za Punde

ZIARA YA RAIS, MKOA WA KASKAZINI PEMBA

Wananchi pamoja na watoto  wa Micheweni waliojitokeza wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamd Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara  ya mazo na bishara na Misitu, Idrissa Hassan Abdalla,alipotembelea kituo cha Msitu wa Ngezi jana,wakiwa katika ziara  ya  siku moja ya Mkoa wa Kaskazini Pemba
 Baadhi ya wananchi na watoto wa Micheweni Pemba wakimsikiliza,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipotembelea mashamba ya kilimo ya wilaya hiyo jana,kuangalia athari za ukame zilivyowaathiri wananchi na mashamba mbali mbali katika wilaya hiyo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Micheweni,Pemba alipofanya ziara ya siku moja katika wilaya hiyo ya Micheweni jana,alipotembelea mashamba ya wakulima na kupata maelezo mbali mbali yanayowahusu wananchi hao,kutokana  na athari za ukame
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisisitiza jambo,wakati alipokuwa akizungumza na Afisa mdhamini Wizara ya Kilimo,Pemba Dk Suleiman Sheikh Mohamed,(wa pili kulia) na Afisa Kilimo Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Maalim Fakih,(wa pili kushoto)na Mama Mwanamwema Shein, alipofanya Ziara ya Kutembelea Mashamba mbali mbali Wilaya ya Wete,yaliyoathirika na Ukame  jana

Picha na Ramadhan Othman, Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.