Habari za Punde

ZIARA YA RAIS MKOA WA KUSINI PEMBA - AKAGUA HALI YA KIANGAZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akiapata maelezo kutoka kwa afisa mdhamini Pemba wa Wizara ya Kilimo na mifugo, Dk Suleiman Sheikh Mohamed, wakati alipotembelea mashamba ya kilimo huko,bonde la kwajibwa, Kengeja, Kusini Pemba, kuangalia athari za kiangazi zilizowakumba wananchi wa maeneo hayo,(watatu kushoto) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein
Wananchi na wakulima  wa Kengeja wakiwa katika bonde la kwajibwa, Mkoa wa Kusini Pemba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na kuwapa matumaini, wakati alipotembelea bonde hilo kuona athari za Kiangazi zilizowakumba wananchi hao jana
Wazazi na watoto wa Kengeja, Kusini Pemba, wakiwa katika bonde la kwajibwa, katika mkutano wa Kuwafariji wananchi hao kutokana na tatizo la mashamba yao kuathirika na kiangazi, na kupelekea kukosa kilimo na wakati huu,walipotembelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akifuatana na Mama mwanamwema Shein, katika ziara hiyo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akipokea malalamiko ya wananchi wa Mwembe Chaleni,kutoka kwa  mwanakijiji  Juma Makame,kutokana na  maeneo ya kijiji chao kuchimbwa mashimo ambayo dhamira yake ni kupata kufusi cha ujenzi wa barabara,mashimo hayo sasa yanajimbuka maji ya chumvi na kuleta wasiwasi mkubwa kwa wananchi maeneo hayo
Ni eneo la mashamba ya Mbuyu hoja, Mwambe Mkoa wa kusini Pemba linaonekana likiwa kavu kabisa kutokana na jua kali la kiangazi na kupelekea wananchi kukosa kilimo kwa wakati huu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akitoa maelekezo kuhusiana na mashimo yaliyochimbwa (Pichani chini) kwa madhumuni ya kupata kifusi cha ujenzi wa Barabara za Mwambe,Kengeja na sehemu nyengine,kuchukuliwa tahadhari kabla kuleta maafa yoyote
Picha na Ramadhan Othman, Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.