Habari za Punde

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KILIVYOPITISHA BAJETI

Ndugu wana Azaki ,

Habari za majukumu yenu ya kila siku, jana hapa wilayani kwetu kulikuwa na kikao cha baraza la madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha wa 2011/2012 nami nilikuwa kwenye kikao hicho ambacho kwangu nilidhani kitakuwa muhimu sana katika kuona na kupima ni vitu gani ambavyo vimepewa kipaumble na halmashauri yangu.Nilichokiona ndugu zanguni ni tofauti na kile nilichokitazamia kukiona na kukisikia, huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyokuwa. Kikao kilikuwa na agenda 4 agenda ya kwanza kufungua kikao, agenda ya 2 kuthibitisha agenda, agenda ya 3 kupokea na kujadili Bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na agenda ya 4 kufunga kikao.

Tofauti na nilivyodhania kwamba madiwani watakuwa na maswali kadha wa kadha ya kuhoji, lakini kikao hicho kilitumia nusu saa kupitisha bajeti hiyo ya shilingi bilioni 34,000,718,593/= ajabu sana.Baada ya kikao kufunguliwa na mwenyekiti alitoa nafasi kwa Kaimu mkurugenzi wa halmashauri kusoma agenda ili zithibitishwe na waheshimiwa madiwani baada ya kuthibitishwa kwa agenda aliitwa mtoa hoja ambaye alikuwa Kaimu Afisa mipango wa wilaya mara baada ya kusoma makadrio ya mapato na matumizi, Hakuna diwani hata mmoja aliyehoji ila wote waligonga meza kuashiria kwamba kila kitu kimepita.

Baadaye alisimama diwani mmoja akasema mheshimiwa mwenyekiti haya mambo wote tnayajua hakuna kipya na ndio maana umeona wote tumekubalina kwamba bajeti hiyo ipite bila kupingwa. Baada ya hapo wenyekiti aliwashukuru wajumbe kwa kuonesha uelewa wa hali ya juu kwa kuipitisha bajeti bila kuipinga akisema hiyo ndiyo kazi nzuri na kisha akaahirisha kikao kuashirika kukamilika kwa kazi.

Cha ajabu sana wakati kikao hicho kikiendelea Wilayani Kigoma tayari mkurugenzi wa halmashauri hiyo na Afisa mipango wake na wakuu wa idara kadhaa ilisemekana walikuwa Dodoma kuwasilisha bajeti hiyo kwa viongozi wa TAMISEMI, hapo niliendelea kushangaa inakuwaje baraza linakaa wakati wanaowasilisha TAMISEMI wameshaondika kufanya hivyo? Niliambiwa na diwani mmoja ambaye hakutaka jina lake lifahamike kuwa huu uliokuwa unafanyika hapa ni kule kufuata formalities tu lakini kila kitu kiliishia kwenye kamati na ndio maana hatukuhoji.

Hata hivyo ndani ya bajeti hiyo kuna mapungufu kadhaa kama kupunguza idadi ya vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja kutoka 25% hadi 15% milioni 24, kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 25% hadi 15% milioni 19. Hivi kupunguza vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja ni nini na kupunguza idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 ni nini? Kupunguza utapia mola miongoni mwa watoto wadogo kutoka 16% hadi 10% Je huu ni mkakati au ni shughuli? Ni shughuli gani ambazo zitafanyika ili kuhakikisha kwamba vifo vya watoto wadogo vimepungua? Hazionekani na wala hakuna aliyehoji, Jamani Halmashauri zetu zina vituko sana! Hivi na ninyi wenzangu halmashauri zenu zinafanya maajabu kama haya?

Wenu katika harakati

Mratibu wa Kioo

KIGOMA

1 comment:

  1. Kumbe wewe ulitarajia nini mwenzentu!!?
    Takriban madiwawani wote ni wezi tu, kama unataliashaka maneno yangu basi mchunguze huyo diwani wa huko unapoishi; uhakika utakuta unasifa ya ubabaishaji na ulaghai, kwani sifa mbili hizi ni muhimu sana mtu kuwanazo ili awezekuwa diwani.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.