Habari za Punde

MWANYANYA KUCHAGUA DIWANI LEO

Na Mwanajuma Abdi

WANANCHI 4,059 wanatarajiwa kupiga kura kesho katika uchaguzi mdogo wa kumchagua Diwani atayeongoza wadi ya Mwanyanya.

Uchaguzi huo unafanywa kufuatia Diwani ya wadi hiyo Haji Hamad wa Chama cha CUF kufariki dunia na kusababisha nafasi hiyo kuwa wazi.

Akizungumza na gazeti hili, Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Magharibi Unguja, Rashid Ali Suluhu alisema uchaguzi utafanyika kesho (Jumapili), ambao utahusisha watu 4,059 kwa mujibu wa daftari la wapiga kura.

Alisema uchaguzi huo utawashirikisha wananchi wanaishi wadi ya Mwanyanya, ambapo kumewekwa vituo saba na Sharifumsa vituo sita na kufanya idadi ya vituo vyote ni 13 vya kupigia kura katika uchaguzi huo.

Aidha alieleza hadi sasa wagombe wa vyama vitatu ndio waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, akiwemo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Hamza Khamis, Chama cha Wananchi CUF Juma Ali na Chama cha CHADEMA kimesimamisha Salum ambae alipatikana kwa jina moja.

Alifahamisha kuwa, vifaa vya uchaguzi vimeshakamilika ambapo leo (Jumamosi) vitasambazwa katika vituo vyote 13 kwa ajili ya zoezi hilo Jumapili.

Hata hivyo, alisema kampeni za uchaguzi hizo zimefanyika kwa kistaarabu kama walivyoagizwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ambapo alitoa wito kwa wananchi wa shehia hizo mbili wenye haki ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi ili kufanikisha uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.