ZFA wilaya ya Magharibi imeelezea kusikitishwa na vitendo vya waamuzi wa wilaya hiyo kushindwa kufika viwanjani kuchezesha mechi wanazopangiwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mshika fedha wa wilaya hiyo, Mwinyimvua Abdi, alisema, waamuzi wamekuwa wakipangiwa mechi lakini bila ya kuwa na sababu maalumu hushindwa kufika viwanjani na hata kutotoa maaelezo ya kushindwa kufika kwao viwanjani.
Alipoulizwa kufuatia kazia hilo uongozi umepanga kufanya nini kwa waamuzi hao wasioelewa wajibu wao, alisema wanatarajia kufanya kikao kujadili mwenendo huo wa waamuzi.
Alisema, pamoja na kujadili suala hilo la waamuzi kutofika viwanjani pia wataangalia na kujadili mwenendo mzima wa ligi hiyo ya Magharibi na kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo ya waamuzi.
" Tumepanga kufanya kikao kujadili suala hili la waamuzi na pia mustakabali mzima wa ligi inavyoendelea" alisema mshika fedha huyo.
Mwinyimvua, alifahamisha kwamba suala la waamuzi kutofika viwanjani kuchezesha mechi kunaigharimu ZFA Magharibi kulipa gharama za klabu na hivyo kupelekea ligi hiyo kutomalizika kwa wakati.
Aidha, ZFA wilaya ya Magharibi imetoa wito kwa klabu kuheshimu sheria 17 za soka pamoja na mchezo wenyewe.
" Vile vile tunaziomba klabu kutoa wachezaji waliostaafu kwa ajili ya kozi ya waamuzi na ZFA wilaya hiyo itagharamia mafunzo hayo" alifahamisha
No comments:
Post a Comment