Na Rajab Mkasaba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema kuwa dawa ya mfumko wa bei ni kuimarisha sekta ya kilimo na kuzalisha kwa wingi vyakula vinavyotumiwa sana na wananchi hapa nchini.
Dk. Shein aliyasema hayo leo katika ukumbi wa Tawi la CCM Kiembesamaki wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Magharibi ikiwa ni mfululizo wa ziara za Mhe. Rais za kuzungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Kutokana na hatua hiyo alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayiri imeshaanza mikakati madhubuti ya kuiimarisha sekta hiyo ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuendeleza kilimo cha mpunga hasa cha umwagiliaji maji sambamba na kuweka fedha nyingi katika kilimo ili kukuza zao hilo pamoja na kujitosheleza kwa chakula.
Alisisitiza kuwa na mazao mengije nayo yataimarisha likiwemo zao la muhogo, mtama, mahindi na mengineyo.
Katika kipindi kifupi cha uongozi wa awamu ya sababu serikali imefanya mambo mengi, yapo yanayoonekana na yapo yasiooneka ambapo yeye mwenyewe binafsi amepata fursa ya kutembelea mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba na kuyaona na kuona haja ya kuwaeleza wanaCCM.
Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaongozwa kwa kufuata Ilani ya CCM sambamba na Dira ya maendeleo ya 2020 ambayo tayari imeshatimia miaka kumi nabado miaka kumi, na katika hatua ya miaka kumi ijayao, kipato cha mtu wa Zanzibar kinatakiwa kisishukuke chini ya Dola 1000.
Dk. Shein aliendelea na kusisitiza yale aliyoyaeleza katika majumuiisho ya ziara yake ya Mikoa iliyomalizika hivi karibuni kuhusu uchafu wa Mji wa Zanzibar na kueleza umuhimu wa kuuweka mji huo safi.
Dk.Shein pia, alieleza utekelezaji wa Ilani ya CCM umekuwa ukiendelea kwa kasi kubwa maendeleoya ujenzi wa skuli mpya za Sekondari Unguja na Pemba na kueleza kuwa ujenzi wa skuli za chekechea nao unaendelea vizuri.
Katika sekta ya kilimo, Dk. Shein alisema kuwa kituo cha Utafiti cha Kzimbani ambacho ndio cha mwanzo cha Afriaka Mashariki na amekipandisha kutoka kituo kuwa Taasisi hiyo ni ktokana na kazi kubwa ya kituo hicho.
Alisema kuwa miongozi mwa kazi kunwa wanayofanya katika kituo hicho ni pamoja na kuanzisha utafiti wa mbeg mpya ya mpunga ya NERIKA ambayo tayari imeshapandwa heka tano za mbegu na baada ya hapo watapewa JKU kwa kuazia heka 100 na baadae kwa wakulima wote na hivi sasa linaandaliwa bonde la Kibondemzungu kwa ajili ya kilimo cha mpunga.
Serikali imeamua kufanya mapinduzi ya kilimo, na kuahidi kuimatrisha kilimo cha kisasa na cha kumwagilia maji kwa bengu bora,, mboea, na kuongeza na kununua matreka mwaka huu na mwakani na kueleza uwa tayari kuna matrekta 50 yapo njiani yanakuja
Alieleza kuwa mbegu mpya zikiwemo za muhogo, mtama, mahindi na nyenginezo na kueleza kuwa katika kipndi kijamcho, tani 80 elfu nai 14, tunaadhima ya kulima hekta 6000 za kilimo cha kumwagilia maji na uwezo wa kutoa tani 4000 elfu hapa Zanzibar.
Tatizo la umeme Mtwango litafanyiwa ufumbuzi na wakulima wataweza kulima mara mbili kwa mwaka na serikali itapeleka pembejeo na vifaa vyengine vya kilimo. Na kueleza kuwa katka bonde la Bumbwisudi tatizo laumeme litapatiwa ufumbuzi wa haraka sanjari na kuimarisha mabonde mengine yote ya Unguja na Pemba.
Wataalamu wasiopungua 104 wataajiriwa katika kipindi hichi cha fedha na kueleza kuwa mbolea, dawa za kuulia magugu.
Tumepitisha sheria mpya ya uhidahi wa chakula, ni lazima tuwe la chakula cha kutosheleza na ndo adhma ya serikali na kwa hilo Zanzibar itawaekezaka na lengo ni kuweka fedha nyingi katika kilimo hasa kilimo cha mpunga. Aidha alisema kuwa tayari hatua za kuweka mbegu bora inachukuliwa.
Alieleza kuwa kutokana na taratibu za kutoa mikopo katika mfuko waMifuko ya JK na AK wananchi waliowengi hawakufaidika a kusisitiza kuwa mifuko hiyo itaimarishwa zaidi na aliwahakaikishia kuwa serikali imo katika mikakati ya kuhakikishwa wananchi wanawezeshwa na kuwaeleza kuwa taratiu pia zitafanyw katika kuanzisha muko wa AS.
Halmashauri zijiendeshe ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zao wenyewe, na kusisitiza kuwa wale waliosababisha matatizo ya arhi wayaamue wenyewe na wakishindwa serikali kuu itawafanyia kazi. Kwa upande wa afya Dk. Shein aliwapongezakwa kuimaarisha sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha afya cha Mbuzini na vyenginevyo.
Ari ya kujitolea hivi sasa haipo na kusisitiza haja ya kuimarisha na kuendeleza hali hiyo na kuwaeleza wanaCCM kuendeleza suala hilo kwa manufaa na kuwasisitiza wanaCCM kusimamia Ilani ya CCM.
Aliwasisitiza viongozi wa CCM kubadilika na kuleta mabadiliko katika CCM kwani wananchi na wanaCCM hawana mbadala katika chama hichi na ni chama cha walio wengi Zanzibar na Tanzania Bara.
Mshikamano ni jambo la lazima na kueleza kuwa ipo haja ya kuendeleza amani na utulivu. Aidha alisema kuwa serikali imo katika kulitafutia ufumbuzi tatizo la ajira kwa vijana.
Nao viongozi wa CCM Wilaya hiyo walimpongeza Dk. Shein kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutoa matumaini kwa wananchi na wanaCCM wa Zanzibar, ziara zake zinawakumbusha kumbukumbu za ziara zake za kampeni na kueleza kuridhika kwao na hatua yake hiyo na kusisitiza kuwa viongozi
No comments:
Post a Comment